In Summary

•Zari alichapisha video zinazomuonyesha akiwa amelala peke yake kitandani na akafunguka anavyotamani mumewe angekuwa karibu naye.

•Haya yanajiri siku chache baada ya Zari na Shakib kuonekana wakitazama fainali za Kombe la Dunia la Raga kati ya Afrika Kusini na New Zealand.

Zari na mumewe Shakib
Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Mwanasosholaiti na mfanyabiashara mashuhuri wa Uganda ambaye anaishi Afrika Kusini, Zari Hassan ameonyesha wazi kuwa ana huzuni.

Hali hii imechochewa na mumewe Shakib Cham Lutaaya kuwa mbali na yeye.

Usiku wa kuamkia Alhamisi, mama huyo wa watoto 5 alichapisha video zinazomuonyesha akiwa amelala peke yake kitandani na katika sehemu ya maelezo, alifunguka jinsi anavyotamani mumewe angekuwa karibu naye.

“Kweli, nam-miss mume wangu,” Zari aliandika kwenye moja ya video na kuambatanisha kauli yake na emoji ya uso wa huzuni kuashiria upweke.

Katika moja ya video hizo, alimrekodi mtoto wake mdogo, Prince Nillan akiwa amelala kwenye kitanda kingine kilichokuwa ndani ya chumba alichokuwemo.

"Prince Nillan akikoroma," aliandika.

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Haya yanajiri siku chache tu baada ya mpenzi huyo wa zamani wa staa wa bongo Diamond Platnumz kuonekana akifurahia muda na mume wake Shakib Lutaaya katika sehemu moja ya burudani nchini Afrika Kusini huku wakitazama mchezo wa fainali za Kombe la Dunia la Raga kati ya Afrika Kusini na New Zealand.

Wanandoa hao hawakuweza kuficha furaha yao wakati timu ys Springboks ya Afrika Kusini iliposhinda All Blacks ya New Zealand katika mechi hiyo ya fainali iliyochezwa nchini Ufaransa Jumamosi.

“Yeess bokkes ilitufanya tujivunie. Hongera @bokrugby #strongertogether,:” Zari aliandika chini ya picha yake na Shakib aliyoiweka Jumapili.

Zari na Shakib walirasimisha ndoa yao katika harusi ya faragha iliyofanyika nchini Afrika Kusini mapema mwezi uliopita. Wawili hao wamekuwa wakichumbiana kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Maelezo ya harusi hiyo yalikuwa yamefichwa sana lakini tulifanikiwa kupata baadhi ya picha na video za sherehe hiyo ya kukata na shoka.

Picha hizo zilionyesha  Zari akiwa amevalia gauni la harusi refu jeupe huku mumewe Shakib akiwa amevalia suti ya kijivu na shati jeupe.

Wanafamilia wakiwemo watoto wa Zari; ; Pinto Tale, George Ssemwanga, Dido Ssemwanga Tiffah Dangote na Prince Nillan walikuwepo kwenye hafla hiyo. Tiffah alivalia gauni jeupe huku Nillan akiwa amevalia suti ya kijivu na shati jeupe sawa na bi na bwana harusi.

Wana wa Zari na aliyekuwa mume wake, Ivan Ssemwanga walionekana wamevalia suti nyeupe, shati jeupe na viatu vyeupe.

Wengi wa wageni waliokuwa wamealikwa kuhudhuria hafla hiyo ya faragha walionekana wamevaa mavazi meupe. Wanaume walikuwa na suti ya kijivu wakati wanawake walivaa gauni za rangi ya dhahabu.

Wawili hao walihalalisha muungano wao wa muda mrefu kwa mara ya kwanza katika harusi ya kidini ya Kiislamu (Nikah) mapema mwaka huu.

View Comments