In Summary

•Zari amejibu maswali kuhusu kwa nini mumewe Shakib Lutaaya anaonekana kukosa furaha mara nyingi  akiwa hadharani.

•Mwanasosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 42 pia alimtetea mumewe kwa kueleza kwamba "Hanaga mambo mengi."

Zari na mumewe Shakib katika eneo la burudani
Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Mwanasosholaiti wa Uganda Zari Hassan amejibu maswali kuhusu kwa nini mumewe Shakib Cham Lutaaya anaonekana kukosa furaha mara nyingi  akiwa hadharani.

Mzazi mwenza huyo wa staa wa bongo Diamond Platnumz alilazimika kuelezea mwonekano wa mumewe hadharani baada ya baadhi ya wanamitandao kugundua sura yake yenye huzuni kwenye chapisho lake la hivi majuzi.

"Lakini mume wako hana furaha, kwa nini?" mtumizi mmoja wa Instagram alimuuliza.

Katika majibu yake, mama huyo wa watoto watano alidokeza kwamba Shakib Lutaaya hucheka tu inapobidi.

"Yeye hacheki bila sababu, ikiwa huoni picha anakocheka basi jaribu tena," alisema.

Shabiki mwingine alimuuliza, "Mbona (Shakib) kanuna?"

Zari bila kusita alijibu, "Hacheki cheki kichizi."

Mwanasosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 42 pia alimtetea mumewe kwa kueleza kwamba "Hanaga mambo mengi."

Licha ya kuwa mzee kuliko yeye, mara nyingi Zari ameonyesha upendo na heshima nyingi kwa mumewe huyo wa miaka 31.

Wiki jana, alifichua kwamba alikuwa na maelezo ya kumfanyia Shakib baada ya kupeperushwa kwa sehemu ya pili ya filamu ya Young, Famous na African (YFA2) ambayo alishirikishwa na mzazi mwenzake, Diamond.

Mapema mwezi huu, Zari aliokeza alichumbiana na Shakib kabla ya kujitosa kwenye ndoa na staa huyo wa Bongofleva.

Katika mahojiano na wanahabari nchini Uganda, mama huyo wa watoto watano aliwathibitisha waandishi wa habari kwamba amemfahamu mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa miaka kadhaa sasa. 

Alikiri kwamba yeye na Shakib walichumbiana miaka kadhaa nyuma kabla ya kutengana na kurudiana tena mwaka jana.

"Nilichumbiana na Shakib huko nyuma kisha tukaenda njia tofauti. Sijui tulipatana vipi tena," Zari alisema.

Mzazi mwenza huyo wa Diamond Platnumz alisema haikuwa ngumu kuungana tena na Shakib na kufunga naye ndoa mwezi uliopita kwani waliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi katika siku za nyuma .

"Mwaka moja baada ya kurudiana alisema nitakufanya mke wangu. Ni hayo tu. Hatukuzungumza kwa muda kisha ghafla mwaka mmoja baada ya kurudiana tukafunga ndoa. Ikiwa sio Mungu, tutaiitaje hiyo?," alihoji.

Zari alirudiana na Shakib mapema mwaka jana baada ya kukatiza mahusiano na mfanyibiashara wa Uganda GK Choppa. Waliweka mahusiano yao siri hadi katikati mwa mwaka jana ambapo walifichua wanachumbiana

View Comments