In Summary
  • Kwenye video hiyo Aristotle aliulizwa kwa kuwa yuko karibu na Diamond na Zuchu ikiwa uhusiano wao ni wa kweli
  • Lakini alijibu akisema kuwa Zuchu huwa anajilazimisha kupendwa na Diamond
ZUCHU NA DIAMOND PLATNUMZ
Image: WASAFI/INSTAGRAM

Zuhura Othman maarufu kama Zuchu amekuwa akigonga vichwaa vya habari kwa muda mrefu zaidi sasa .

Hii ni kufuatia uhusiano wake katika WCB Wasafi,  Diamond Platinumz.

Wawili hao wamedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi tangu mapema mwaka jana. Walakini, hakuna yeyote kati yao ambaye amejitokeza kuthibitisha au kukanusha uvumi huo.

Leo kwenye mojawapo ya kurasa za blogu maarufu Tanzania video ya Aristotle imepakiwa. Aristotle ni rafiki wa karibu wa Diamond ambaye amekuwa akifanya kazi na Diamond Platinumz tangu mapema hata kabla ya umaarufu.

Kwenye video hiyo Aristotle aliulizwa kwa kuwa yuko karibu na Diamond na Zuchu ikiwa uhusiano wao ni wa kweli.

Lakini alijibu akisema kuwa Zuchu huwa anajilazimisha kupendwa na Diamond.

Aristotle aliongeza kuwa Diamond hajawahi kuridhika na hilo kwa sababu anawaheshimu wafanyakazi wake.

View Comments