Msanii wa nyimbo za bongo kutoka Tanzania Lava Lava na ambaye amesajiliwa katika lebo ya wasafi ambayo ni staa wa bongo Diamond Platnumz ametoa kibao kipya kinachofahamika kama 'Wale wale'.
Kibao hicho kinazungumzia jinsi alikuwa na mpenzi na kisha akamtoka na kumuendea sponsor.
Licha yake ya kumuendea sponsor mpenzi huyo alianza kuenda katika sheherehe za usiku kwenye klabu.
Pia kinazungumzia jinsi alimuua sponsor wa mpenzi wake huku akitiwa ndani kwa kosa la mauaji.
Baada ya kufungwa alipitia changamoto akiwa jela, huku akimlaumu mwanamke huyo kwa kuto mwambia ukweli kuhusu mapenzi yao.
Ni kibao ambacho kimepokea watazamaji zaidi ya elfu 56 kwa saa saba zilizopita.
Hii hapa video ya kibao hicho