In Summary

•King Kaka alifichua kwamba alipokuwa katika darasa la nne alishambuliwa na ugonjwa hatari ambao ulimfanya ajikune mwili wote mara kwa mara kiasi cha kwamba angemwaga ngozi.

•Alieleza kwamba hatimaye aliweza kupata afueni baada ya kutumia dawa ambayo kwa kawaida watu walitumia kujichumbua ngozi.

Image: INSTAGRAM// KING KAKA

Rapa mashuhuri Kennedy Ombima almaarufu kama King Kaka amefunguka kuhusu maisha yake ya utotoni.

Akiwa kwenye mahojiano na Mwafreeka katika kipindi cha 'Iko nini' mwanamuziki huyo alifichua kwamba maisha yake ya utotoni hayakuwa nyororo kwani kwa kipindi kirefu alipambana na ugonjwa wa ngozi wenye kutisha.

King Kaka alifichua kwamba alipokuwa katika darasa la nne alishambuliwa na ugonjwa hatari ambao ulimfanya ajikune mwili wote mara kwa mara kiasi cha kwamba angemwaga ngozi.

"Tangu nikiwa katika darasa la nne, kila mwaka nilikuwa namwaga ngozi kama nyoka. Tulishindwa kutambua ni nini. Ilikuja ikaisha tu yenyewe. Ilikuwa noma, nilikuwa najikuna viungo vya mkono na miguu, hivyo ndivyo viliathirika zaidi. Kadri nilivyojikuna zaidi nilianza kuvunja damu" King Kaka alisema.

Mwanamuziki huyo alisema kwamba juhudi zao zote za kutafuta tiba ziliangulia patupu licha ya wao kutembelea hospitali na wataalamu wengi.

Alieleza kwamba hatimaye aliweza kupata afueni baada ya kutumia dawa ambayo kwa kawaida watu walitumia kujichumbua ngozi.

"Tulienda kwa madaktari wa ngozi tangu niwe mdogo. Tulitembea kwa wahindi na madaktari wengine. Kuna  dawa ilikuwa maarufu ambayo watu walitumia kujichumbua ngozi, hiyo ndiyo ilinisaidia. Iliharakisha kupona kwangu" Alifichua.

King Kaka alieleza kwamba ugonjwa huo hata  ulimzuia kujiunga na shule ya upili ambayo alikuwa ameitwa kwa muda wa kujiunga ulikuwa umeisha.

View Comments