In Summary

• Staa wa muziki ambaye pia ni mwanabiashara huko Tanzania, Wema Sepetu amemjibu Aristote baada ya kusema kuwa msanii huyo hana gari na kwamba bado anatumia uber katika usafiri.

• Kwa upande wake Sepetu amesema kwamba hayupo kwenye ushindani na mtu yeyote na kwamba anafanya kila kitu maishani mwake katika wakati wake.

• Katika sikun za hivi karibuni kumeonekana mtindo wa kuwafananisha wasanii mbalimbali huku washikadau na mashabiki wakijiuliza iwapo hilo litakuwa jambo la kujenga au kubomoa sanaa ya Tanzania.

Staa wa muziki ambaye pia ni mfanyibiashara huko Tanzania, Wema Sepetu amemjibu Aristote baada ya kusema kuwa msanii huyo hana gari na kwamba bado anatumia uber katika usafiri.

Hili linajiri siku chache baada ya Aristote kumfananisha Sepetu na mwanafilamu Irene Uwoya ambaye walikuwa wakijiburudisha naye katika mji wa Arusha, huku akionekana kutumia hela nyingi katika ‘ulaji bata’. Aristote alisema kwamba Wema Sepetu hawezi kuyakimu maisha kama yale ya Uwoya kwani kiwango chake bado kipo chini.

“Wacha nikuweke kabisa kwa page yangu upate kufurahi...maana nimekaa sana mdomoni mwako...kutwa huishi kunitaja. Kurequest nako ni K vile maana nakutanaga na mashabiki pia nikiwa kwenye uber na Bolt, and by the way, miaka miwili sasa sina gari na mbona maisha freshi tu...Mkitembea nyinyi ma Range inatosha Aristotee.. sio mbaya,” alisema Wema Sepetu.

Kwa upande wake Sepetu amesema kwamba hayupo kwenye ushindani na mtu yeyote na kwamba anafanya kila kitu maishani mwake katika wakati wake, na kubwa zaidi kuwa bora kuliko jana hivyo basi Aristote akome kumfananisha na wasanii wengine wa filamu kutoka bongo.

Mashabiki wengi wamejitokeza kwenye ‘comment section’ kusema jinsi gani wasivyompenda Aristotee na kuonekana kumshabikia Wema Sepetu huku wakimrai kuendelea kushughulikia maisha yake bila kujali wanachokisema watu wengine.

Katika sikun za hivi karibuni kumeonekana mtindo wa kuwafananisha wasanii mbalimbali huku washikadau na mashabiki wakijiuliza iwapo hilo litakuwa jambo la kujenga au kubomoa sanaa ya Tanzania.

View Comments