In Summary

• Msanii chipukia Diana Marua amekiri kuwa atakuwa anasajili msanii mgeni kwenye lebo ya Diana B entertainment.

•Kwa upande wake Kevin Bahati ambaye ni mpenzi wake, ameonekana kushabikia hatua hiyo  huku akisema kwamba anaaminia Diana Marua atatimiza mengi na mkubwa katika muziki.

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Msanii chipukia Diana Marua amekiri kuwa atakuwa anasajili msanii mgeni kwenye lebo ya Diana B entertainment.

Diana Marua ambaye hajamaliza mwaka mmoja tangu aingie katika usanii, anaonekana kuwa na ari ya kufanya kila kitu kupeleka muziki wa Kenya katika viwango vya kimataifa. Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Marua alimkaribisha Vinny Flava kwenye gemu la burudani hapa nchini na kuahidi mashabiki kwamba watazidi kuwapa viwango vya juu vya burudani.

“My record label Diana b entertinment welcomes my 1st signed artist @vinnyflava lets change the music industry forever!!!!” aliandika Diana Marua.

Mashabiki wameonekana kupendezwa na hatua hiyo huku wakisubiri kwa hamu kuona kazi zitakazotolewa chini ya lebo hiyo mwaka huu wa 2022.

Kwa upande wake Kevin Bahati ambaye ni mpenzi wake, ameonekana kushabikia hatua hiyo  huku akisema kwamba anaaminia Diana Marua atatimiza mengi na mkubwa katika muziki.

Ikumbukwe kwamba hili linajiri siku chache tu baada ya Marua kufanikiwa kurejesha akaunti yake ya YouTube ambayo ilikuwa imedukuliwa na video zake kufutwa.

Mashabiki wanasalia na maswali mengi iwapo utakuwa ni wakti mwafaka kwa Marua kusign msanii ilihali hajakomaa katika muziki wa Kenya, huku wengi pia wakisubiria kuona biashara ya muziki ikifahamika kwamba mumewe pia ana leo yake [EMB records].

 

 

 

View Comments