In Summary

• Vincent Mboya, jamaa aliyekejeliwa na KRG the Don Pamoja na Eddie Butita ameamua kujibu madai hayo kwa kwikwi.

• Akizungumza na mjenga maudhui Mich Guy, Mboya ametoka na machozi huku akijaribu kujieleza jinsi ambavyo alichukulia maneno ya kashfa kutoka kwa KRG na Butita.

Image: HISANI

Vincent Mboya, jamaa aliyekejeliwa na KRG the Don Pamoja na Eddie Butita ameamua kujibu madai hayo kwa kwikwi.

Mboya alionekana kwenye mkutano wa wawili hao ambao walikuwa wanazungumza wa wakuza maudhui ila KRG na mwenzake Butita walimuapiza na kumkejeli kwa njia ambayo ilizua kashfa kali mitandaoni dhidi ya wawili hao.

Akizungumza na mjenga maudhui Mich Guy, Mboya ametoka na machozi huku akijaribu kujieleza jinsi ambavyo alichukulia maneno ya kashfa kutoka kwa KRG na Butita.

Katika video ya awali ambapo wawili hao wanamsukuma na kumtupia maneno makali Mboya hadharani mbele ya kamera, KRG alisikika na kuonekana akimdhalilisha kwamba yeye ni maskini jeuri ambaye hawezi saidika huku Butita akipiga msumari wa mwisho kwenye jeneza lake kwa kusema kwamba Mboya ni asilimia 75 mshamba na pia hana akili timamu.

Mboya ambaye wakati huo alionekana katulia ameibuka Februari 10 na katika mazungumzo na Mich Guy ameshindwa kujizuia mbele ya kamera akieleza jinsi ambavyo masimango hayo yalimfika.

“Lakini sasa mkienda mahali mnaniita takataka sijui mnanifanya nini, ni sawa. Mi najua kunaye Mungu yuko mbinguni,” alisema Mboya huku akizidiwa na machozi.

Ikumbukwe hii haikuwa mara ya kwanza kwa mchekeshaji Eddie Butita kumdhalilisha hadharani kwani wiki iliyopita Butita alimfukuzia mbali kwenye tamasha ya siku ya kuzaliwa ya mchekeshaji YY na mboya alipoulizwa tatizo lake na Butita kiini chake ni kipi, alikuwa na haya ya kusema,

“Mimi Nairobi sina shida na mtu yeyote ndugu yangu. Mimi sina beef na mtu, kitu ninafanya ni mimi najaribu sana kusukuma Maisha tu”

View Comments