In Summary

• Msanii Willy Paul amekiri kwamba baadhi ya kiki zinapangwa na wasanii wenyewe ili kusukuma miziki yao kufikia watu wengi.

• Pozze amewaomba radhi mashabiki wake kwa wakati wote ambao amefanya kiki ili kusukuma ngoma zake na kuwahakikishia kwamba atakuwa anatia bidii zaidi kutoa ngoma nzuri zinazojiuza bila kiki.

Willy Paul
Image: Instagram/willy paul

Msanii Willy Paul amekiri kwamba baadhi ya kiki zinapangwa na wasanii wenyewe ili kusukuma miziki yao kufikia watu wengi.

Kupitia ujumbe alioachia katika ukurasa wake wa Instagram, Pozze amewaomba radhi mashabiki wake kwa wakati wote ambao amefanya kiki ili kusukuma ngoma zake na kuwahakikishia kwamba atakuwa anatia bidii zaidi kutoa ngoma nzuri zinazojiuza bila kiki.

“Samahani mashabiki wangu, mwaka huu ni pure music,” aliandika Willy Paul.

 Kwa upande wa mashabiki, wameonyesha kukerwa na hali hiyo huku wakisema kwamba wasanii wamekuwa wakiwachukulia poa kwa muda mrefu huku wakwarai kujikita katika kufanya muziki mzuri bila kiki.

Aidha kuna wale walionekana kumkashifu Willy Paul wakisema kwamba manii huyo hawezi kufanya vizuri katika burudani la humu nchini bila kiki.

Swala ambalo kwalo wengi wanazidi kujikuna vichwa ni iwapo ile kesi ya Willy Paul kujaribu kumnajisi Diana Marua ilikuwa kweli ama miongoni mwa kiki zake za kawaida.

Kwa sasa mashabiki watalazimika kusubiri kuona iwapo msanii huyo atatimiza ahadi aliyotoa kwao kadri siku zinavyosonga.

 

View Comments