In Summary

• Msanii Bahati amesema kwamba ataacha muziki iwapo mke wake, Diana Marua atakuwa signed na lebo ya Universal.

• Aidha Bahati amesema kwamba atafanya kila kitu kuhakikisha kwamba mkewe anapata kila atakacho kuzidi kufanikisha kipaji chake cha kuimba.


 

Image: INSTAGRAM// BAHATI

Msanii Bahati amesema kwamba ataacha muziki iwapo mke wake, Diana Marua atakuwa signed na lebo ya Universal.

Akizungumza na wanahabari, Bahati amekiri kwamba msanii Diana B amekuwa akifanya vizuri kimuziki katika siku za hivi karibuni, na kwamba tayari kuna mazungumzo kati yao na lebo za Sony na Universal ili  kusimamia muziki wake na iwapo hilo litaenda sawa basi atalazimika kuacha muziki.

Aidha Bahati amesema kwamba atafanya kila kitu kuhakikisha kwamba mkewe anapata kila atakacho kuzidi kufanikisha kipaji chake cha kuimba.


Kulingana na Bahati ni kwamba Diana B amefanikiwa kuwa na wafuasi wengi kuliko wasanii wengi waliodumu kwenye gemu kwa muda mrefu huku akiwaahidi mashabiki kuwa ndio mwanzo wa mambo makubwa kutoka kwa msanii huyo.

Kwa sasa inasubiriwa kuona Diana B ataafikiana na lebo gani ili kupeleka muziki wake kimataifa.

View Comments