In Summary

• Msanii na mcheza santuri maarufu wa ngoma za Mugithi nchini Kenya DJ Faxto aliwazawidi wazazi wake nyumba ya kifahar

• Mcheza santuri huyo pia ameweka wazi kwamba wazazi wake ndio wamekuwa nguzo muhimu ya mafanikio yake Pamoja na msukumo wa kufanya mema katika mishe zake.

Msanii na mcheza santuri maarufu wa ngoma za Mugithi nchini Kenya DJ Faxto aliwazawidi wazazi wake nyumba ya kifahari kama njia moja ya kuwasherehekea kwa malezi mema siku kuu ya wapendanao.

Mcheza santuri huyo amewashukuru wazazi wake, haswa mama yake kwa kumfunza kuwa mpole na muungwana kwa kila mtu , na babake kwa kumfunza kuwa jasiri wakati wa majaribio magumu.

“Ahsante sana mama kwa kunifunza unyenyekevu na baba kwa kunifunza kuwa jasiri wakati mambo ni magumu. Nina deni kubwa kwenu nyote wazazi wangu. Kila kila nimesoma katika Maisha kinatokana kwenu,” aliandika Faxto

Mcheza santuri huyo pia ameweka wazi kwamba wazazi wake ndio wamekuwa nguzo muhimu ya mafanikio yake Pamoja na msukumo wa kufanya mema katika mishe zake.

“Kukuza kijana kama mimi ingekuwa vigumu sana kama hamngekuwa na malezi ya kupigiwa mfano. Ahsante sana kwa kuwa na Subira na mimi. Nawapenda wote baba na mama,” amewalimbikizia hongera wazazi.

Awambia wazazi wake kwamba kama kungekuwa na nafasi ya kuishi tena Zaidi ya mara moja katika Maisha, basi yeye angechagua tena na tena kuwa mtoto wao.

“Ahsante kwa kuwa nyumba yangu. Heri njema za siku ya valentino wazazi wangu wapendwa na tafadhali pokea hii zawadi yangu kidogo,” aliandika Faxto huku akiwapokeza nyumba hiyo.

View Comments