In Summary

• Msanii Nameless ameeleza jinsi marehemu E-Sir alivyomsaidia kukwepa kifo wakati wa ajali ambayo iligharimu Maisha ya msanii huyo

• “Ndugu yangu E-Sir, ninahisi kwamba niko na hadithi ya kueleza kuhusu kifo chake na jinsi alivyonitoa katika viti viwili ambapo nimekufa kwa ajali hiyo," alisema Nameless

 

Image: HISANI

Msanii Nameless ameeleza jinsi marehemu E-Sir alivyomsaidia kukwepa kifo wakati wa ajali ambayo iligharimu Maisha ya msanii huyo

Akizungumza katika uzinduzi wa Pride of Kenya, Nameless amesema kwamba E-Sir alikuwa anamchukulia kama kakake na kumsaidia kukwepa ajali ambayo ingegharimu Maisha yao wote.

“Ndugu yangu E-Sir, ninahisi kwamba niko na hadithi ya kueleza kuhusu kifo chake na jinsi alivyonitoa katika viti viwili ambapo nimekufa kwa ajali hiyo.  Yeye ndiye aliyenitoa hapo bila mimi kujua kwamba alikuwa ananitumia ujumbe wa ‘hapana, tukae kwingine’. Kila mara nikikumbuka kisa kile huwa ninahisi nina jukumu kubwa la kuzungumza na kila mara huwa najiuliza mbona Mungu akaruhusu vile,” alisema Nameless

Msanii huyo mkongwe kwenye tasnia ya muziki nchini ambaye hivi karibuni ametoa ngoma ya kusherehekea Maisha ya E-Sir, mradi ambao aliwashirikisha wasanii wenza na kuita ‘Bandana ya E-Sir’ amewashauri wasanii wanaochipukia kuiga mfano wa E-Sir kwani alikuwa ni mtu mwema, mnyenyekevu na wa kujituma sana kimuziki.

“Kuwa mnyenyekevu inamaanisha uko wazi kusikiliza na kupokea mawazo mengine, mtu mnyenyekevu huwa hajihisi kwamba anajua kila kitu na hiki ndicho kilimfanya E-Sir kukua haraka kimuziki kwa sababu alikuwa anasoma tasnia haraka. Na hicho ndicho kitu ningependa kuwafunza wasanii chipukizi,” aliwusia Nameless

View Comments