In Summary

•Ameeleza kuwa muziki wa Gengetone unaendelea kukua kwa kasi na ni  miongoni mwa nyimbo ambazo zinaendelea kupendwa zaidi wakenya.

•Amejitolea zaidi kuhakikisha muziki wa Gengetone unafika mbali na kuhakikisha wanaoupiga  mawe muziki huo wamekoma na kuunga mkono kuboresha vipaji vya vijana wa humu nchini.

Mejja
Image: Hisani

Mwanamuziki nguli wa nyimbo za Gengetone Mejar Nameye Khadija almaarufu Mejja ameeleza kuwa muziki wa Gengetone unaendelea kukuwa kwa kasi na ni  miongoni mwa muziki ambao unaendelea kupendwa zaidi na wakenya.

Kupitia mahojiano na kutuo kimoja redio nchini Mejja alieleza kuwa  ni kinaya kuona baadhi ya wanahabari   wakieneza uongo kuwa muziki wa Gengetone unaendelea kufifia huku wakitoa maoni hasi kuhusu muziki huo.

"Hakuna mahali  wanakwama, Arusha wanasikiza Gengetone sana, napigiwa simu na hawa  wasanii wa Uganda na Tanzania wakitaka  mdundo wa Gengetone, Wakenya wanapenda Genge ingekuwa hawapendi genge singekuwa  naimba, ni watangazaji   wachache waliweka kasumba mbaya kwa akili za watu,  watu ndio waliweka hiyo kasumba mbaya ,”alisema Mejja.

Mejja alitoa kibao cha kwanza mwaka wa 2007 ambacho kilikuwa kinatambulika kama 'Landlord' na tangu hapo amekuwa akitunga nyimbo ambazo zameibuka kupendwa sana  na wakenya.

Aliongeza kuwa amejitolea zaidi kuhakikisha muziki wa Gengetone unafika mbali na kuhakikisha wanaoupiga  mawe muziki huo wamekoma na kuunga mkono kuboresha vipaji vya vijana wa humu nchini.

"Wanafaa wajue hawa wasanii wa gengetone ni vijana hakuna vile kijana atafikiria kama wewe mzee umekomaa, sasa wewe mtu umekomaa ukianza kuwatusi si vizuri. Mnafaa kuonyesha hawa vijana njia na si kuwatusi,” Alisema Mejja.

View Comments