In Summary

• Iyanii ameshinda tuzo ya msanii bora anayechipukia kwenye sanaa ya muziki nchini Kenya na kusemac kwamba sanaa ya Kenya inaendelea kuinuka na itashinda Grammy na B.E.T 

Iyanii
Image: Hisani

Msanii Iyanii ambaye hana muda mrefu tangu kujiunga kwenye Sanaa ya muziki nchini Kenya tayari juhudi zake zimesikika na wengi ambapo amezawidiwa tuzo mbili katika tamasha ya Pulse Music Video Award iliyoandaliwa kwenye mgahawa wa Nairobi Street Kitchen usiku wa Alhamisi 24.

Msanii huyo ambaye wengi walimjua na wimbo wake wa kwanza kabisa kwa jina Pombe, ametuzwa zawadi mbili za PMVA ambapo ametambuliwa kama msanii bora anayechipukia kwenye Sanaa ya muziki nchini ‘Breakthrough Artiste of the Year’ na vilevile amepokezwa zawadi nyingine ya kuwa chaguo bora la watazamaji, ‘Viewers’ Choice Award’.

Iyanii amesifiwa na wengi kwa kutoka vibao ambao vinaendana na maudhui ya wapenda tafrija ambap baada ya kibao cha Pombe ametoa vibao vingine, cha hivi karibuni kikiwa cha Valentino.

Msanii huyo amewashukuru mashabiki na wafuasi wake kwa kumuamini na kura zao na kuwaahidi kwamba ndio mwanzo mkoko unaalika maua kwani mambo mengi mazuri yapo njiani yanabisha kwenye Sanaa ya muziki nchini.

“Niko na furaha sana leo, ningependa kusema big shout out kwa watu wangu manze kwa kunipigia kura. Ndio hizi awards manze, tumezileta mtaani. Ninataka kusema ahsante sana kwa kila mtu aliyeniaminia. Pia ningependa kusema huu ni mwanzo tu kwa muziki wa Kenya. Endeleeni kusapoti muziki wa Kenya kwa sababu tuna nafasi kubwa sana na tunaenda kushinda. Grammy tunakuja, B.E.T tunakuja pia na safari hii muziki wa Kenya unaenda kupata heshima inayostahili,” alisema Iyanii katika video aliyoiweka Instagram yake.

View Comments