In Summary

• Wanamuziki na watangazaji mbalimbali katika taifa la Tanzania walipelekea katika mitandao yao ya kijamii kumsherehekea marehemu Ruge Mtahaba.

• “ Endelea kupumzika kwa amani kakangu, mhamasishaji na bosi wangu wa daima ,” aliandika B Dozen.

Ruge Mtahaba
Image: Instagram KWA HISANI

Wanamuziki na watangazaji mbalimbali katika taifa la Tanzania walipelekea katika mitandao yao ya kijamii kumsherehekea marehemu Ruge Mtahaba.

Ruge Mtahaba alikuwa ni mshikadau wa burudani ambaye aliwashika mkono wasanii wengi kama vile Nandy, Diamond Platnumz na Baranaba Classic.

Kauli hizo zilijiri ikiwa ni miaka mitatu tangu Ruge akutane na mauko yake, huku wengi wakimtaja kama shujaa wa muziki wa Bongo.

“ …Bosi wangu, jasiri, Mungu ana sababu zake,” aliandika mtangazaji Millard Ayo.

“ Endelea kupumzika kwa amani kakangu, mhamasishaji na bosi wangu wa daima ,” aliandika B Dozen.

Mtahaba alikuwa mwanzilishi wa ‘Tanzania House of Talent’ almaarufu THT, ambayo ilijikita katika kutoa mafunzo ya muziki kwa wasanii chipukizi.

Pia alikuwa na mchango mkubwa katika tamasha la Tigo Fiesta ambalo liliandaliwa na kituo cha habari cha Clouds Media Group.

 

View Comments