In Summary

• Hatimaye Kim Kardashian amevunja rasmi mahusiano yake na Kanye West baada ya mahakama kukubali ombi lake la kutangazwa wazi kuwa single na kulitoa jina la West kwenye stakabadhi zake.

BBC News
Image: Gatty Imagess

Baada ya muda mrefu wa kuvurugana katika ndoa yake na msanii Kanye West, mwanamitindo Kim Kardashian sasa ni rasmi kuwa amehalalishwa kulifutilia mbali jina la West kwenye stakabadhi zake baada ya kushinda kesi aliyoiwasilisha mahakamani kutaka kutangazwa rasmi kuwa single na hayupo tena na Kanye West.

Kesi hiyo ambayo aliiwasilisha mahakamani mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuachana ilipata pingamizi kubwa kutoka kwa Kanye West ambaye alikataa kabisa Kardashian kutangazwa kuwa single kwa kile alichokisema bado anampenda na hata kumtaka arudi ili wazidi kulea wanao Pamoja, jambo ambalo Kardashian alikataa kabisa na kuendelea mbele na kesi ya talaka na kutanga iwekwe rasmi kwamba hayupo katika mahusiano na West tena.

Wawili hao wamekuwa katika mahusiano ya ndoa tangu mwaka wa 2012 na kubarikiwa na watoto wanne lakini mwaka jana Kardashian alimtuhumu Kanye West kwa kile alisema ni unyanyasaji na hivyo kuelekea mahakamani ili kutaka ndoa yao ivunjwe na kudai talaka yake, jambo ambalo West alilipinga wazi na kusema kwamba angependa sana kuwa na familia yake Pamoja.

Kanye West ambaye Jumatano ametangazwa kuwa rapa wa pili kote ulimwenguni kwa marappa waliovuna pakubwa mwaka 2021 kutokana na kazi zao za muziki kwa siku za hivi karibuni ameonekana kuwa na unyongovu na msongo wa mawazo kutokana na kuvunjika kwa ndoa yake, mpaka wakati mmoja akasikika akiomba Mungu amrudishie furaha katika familia yake kama ambavyo imekuwa kwa miaka kumi ya awali.

View Comments