In Summary

• Alex Mathenge amewataka watu waache kutumia mzaha wa 'kwani sisi ni wanawake' kwa sababu kwake anaona ni kauli ya kuwakera wanawake.

• Aliwata watu kuwaheshimu wanawake kwa sababu sisi wote tumetoka kwao.

Alex Mathenge
Image: Facebook

Mchekeshaji Alex Mathenge amedhihirisha wazi jinsi ambavyo amechukizwa na ‘meme’ ya “kwani sisi ni wanawake” inayozidi kusambaa mitandaoni kama moto wa msitu jangwani na kusema kwamba mzaha huo si kitu cha kuchekesha bali ni maneno ya kuwadhalilisha wanawake.

Akiandika kwenye Instastories zake, Mathenge amesema mzaha huo hata haufurahishi kama vile watu wengi ambao wamekuwa wakiusambaza mitandaoni wanadhani, huku wakiutumia karibia kwa kila maneno wazungumzayo na kumaliza kwamba ‘kwani mimi ni mwanamke’

“Huo mzaha wa ‘kwani sisi ni wanawake’ inakera sana na ni kama kuwadhalilisha na kuwadunisha wanawake. Ni vizuri kuheshimu wanawake kwa sababu sisi wote tulitokana nao. Ni jukumu letu sisi wote kuwaheshimu mama zetu, dads zetu, wake zetu na hata wapenzi na marafiki zetu wa kike. Na si kwamba nawatetea,” aliandika Mathenge kwenye msururu wa instastories.

Mchekeshaji huyo ambaye anaigiza kama polisi pia aliwaacha wengi katika kicheko baada ya kukana kwamba hawatetei wanawake lakini wakati huo huo akitumia maneno yayo hayo ambayo ameyakemea.

“Ati nawatetea, kwani mimi ni mwanamke,” aliandika Mathenge.

Baadae alifichua kwamba wanaume wamefurika katika DM yake kumpa msomo wa karne kuhusu maneno yake hayo kwamba mzaha huo unadhalilisha wanawake. Aliwaonya kukoma kujaa kwenye DM yake kwa sababu yeye alizungumza mawazo yake tu kwamba maneno hayo kwake yanatamkika kama kukera kwa wanawake.

“Wanaume token kwenye DM yangu. Nilisema mzaha huo nauona kama wa kukera kwa wanawake! Kwani nyinyi ni wanawake?” aliuliza Mathenge.

View Comments