In Summary

• Jalang'o apakia picha akiwa na viatu vyenye nembo ya chama cha ODM, wengi wamshabikia kwa msimamo mkali katika chama hicho.

Jalang'o
Image: Instagram

Mtangazaji na mwanasiasa Jalang’o amewaacha wengi wakimsifia mitandaoni baada ya kupakia picha akiwa amevalia viatu vyenye nembo ya chama cha ODM.

Jalang’o ambaye mwezi jana ametangaza kujiuzulu redioni na kujitupa kwenye siasa akilenga kuchaguliwa kama mbunge wa Lang’ata amepakia picha hiyo na kusema kwamba ni sehemu ya maandalizi ya kampeni za kinara wa Azimio la Umoja Raila Odinga kuelekea Magharibi mwa nchi.

“Jeshi ya baba tunakuja Bungoma,” aliandika Jalang’o kwenye picha hiyo aliyoipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mtangazaji huyo ambaye amejiongeza kama mwanasiasa na mfanyibiashara pia amesifiwa nac watu wengi sana huku hadithi ya maisha yake jinsi alivyoanza kutoka chini mpaka kujipata akila kwenye meza moja na watu wenye majina makubwa, imegusa wengi huku ikimlimbikizia sifa sufufu za kuwa mfano wa kuiga katika suala zima la bidi na jitihada.

Jalang’o anatarajia kupambana katika mchujo wa chama hicho ili kuwania tikiti ya chama cha ODM akitarajia kumshinda mshindani mkuu katika eneo bunge hilo ambaye pia ni mbunge wa sasa ,Nixon Korir.

 

 

View Comments