In Summary

•Bahati amtakia mkewe kheri za siku ya wanawake huku akimtaja kama mwanamke wa ajabu ambaye amekuwa akimtunza vizuri kila siku. 

•Bahati na Diana wamekuwa pamoja kwa kipindi cha takriban miaka sita na wamebarikiwa na watoto wawili pamoja.

Image: INSTAGRAM// BAHATI KENYA

Siku ya Jumanne dunia yote iliadhimisha 'Women's Day'.

Walimwengu walitumia fursa hiyo kuwatambua wanawake muhimu maishani mwao wakiwemo mama, wake, dada na mabinti zao.

Mwanamuziki wa nyimbo za kisasa Kelvin Kioko almaarufu Bahati alimsherehekea mkewe na mama ya watoto wake wawili Diana Marua.

Bahati amtakia mkewe kheri za siku ya wanawake huku akimtaja kama mwanamke wa ajabu ambaye amekuwa akimtunza vizuri kila siku. 

Mwanamuziki huyo ambaye alilelewa katika makao ya watoto yatima baada ya kumpoteza mamake mzazi alisema anatamani sana mzazi wake angekuwa hai ili apate nafasi ya kupatana na mkaza mwanawe.

"Siku zote huwa Natamani Mama Angekuwa hapa kukutana na mwanamke huyu mzuri ambaye amekuwa akimtunza mwanae kila wakati ❤ Heri za siku ya wanawake mke wangu wa ajabu Diana Marua," Bahati aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Bahati alimpoteza mamake mzazi akiwa na umri mdogo wa miaka saba. Baada ya mamake kufariki mwanamuziki huyo alichukuliwa na ABC Children's Home ambako alilelewa.

Bahati na Diana wamekuwa pamoja kwa kipindi cha takriban miaka sita na wamebarikiwa na watoto wawili pamoja. 

Diana pia alimpoteza mamake zaidi ya mwongo mmoja uliopita.

View Comments