In Summary

•Mwanamuziki huyo kutokea eneo la Kati alisema huwa anatunga nyimbo zake kulingana mienendo ya kisiasa.

•Alifichua kuwa alikabiliana na upinzani mkubwa mno wakati alipomtungia kinara huyo wa ODM wimbo wa kampeni.

Ben Githae katika studio za Radio Jambo mnamo Februari 2019
Image: RADIO JAMBO

Mwanamuziki wa nyimbo za injili na za kisiasa Ben Githae amefunguka kuhusu funguka kuhusu ushiriki wake katika siasa za kitaifa.

Akizungumza katika Citizen TV hivi majuzi, Githae alisema nyimbo zake zilianza kutumika siasani mwaka wa 2007.

Mwanamuziki huyo kutokea eneo la Kati alisema huwa anatunga nyimbo zake kulingana mienendo ya kisiasa.

"Kuna mienendo ya siasa. Wakati ule (2017)  niliposema tano tena watu wetu walisema Ben ako juu sana. Wakati walianza kuona kama Uhuru kama hawapeleki vizuri walianza kunipiga wakisema hii tano tena  ndio ilituletea hizi shida zote. Ni kwa sababu mienendo huwa inabadilika," Githae alisema.

Githae ambaye aliwapigia debe sana Uhuru na Ruto katika uchaguzi mkuu wa 2013 na 2017 alisema amechagua mwenyewe kumuunga mkono Raila Odinda katika uchaguzi wa mwaka huu.

Alifichua kuwa alikabiliana na upinzani mkubwa mno wakati alipomtungia kinara huyo wa ODM wimbo wa kampeni.

"Mimi niliamua nitaenda na Raila mpaka mwisho hata kabla Uhuru aseme. Nilipokuja nikasema 'mlima wote, baba tosha', Wakikuyu wengine waliniambia sasa kwani uko na mlima yako? ni mlima gani unasema? Unatusemea kwa nini?," Githae alisema.

Mwanamuziki huyo alisema wimbo wake umesaidia waziri huyo mkuu wa zamani kupata umaarufu mkubwa katika eneo la kati.

View Comments