In Summary

• Msanii kutoka Tanzania, Harmonize amempigia magoti Madam Rita kama njia moja ya kutoa shukran zake kwa kumsaidia kujenga kipaji chake.

• “Sio lazima mtu akuambie yes ndo usaidike, anaweza akakuambia no na akawa amekusaidia. Niseme kweli, hakungekuwa na Kondeboy bila Madam Rita,” Harmonize alisema.

Instagram, KWA HISANI
Image: Harmonize

Msanii kutoka Tanzania, Harmonize amempigia magoti Madam Rita kama njia moja ya kutoa shukran zake kwa kumsaidia kujenga kipaji chake.

Hili lilitokea katika hafla ya Serengeti Festival iliyofanyika mjini Dodoma, huku Harmonize akionyesha hisia nyingi jukwaani.

“Sio lazima mtu akuambie yes ndo usaidike, anaweza akakuambia no na akawa amekusaidia. Niseme kweli, hakungekuwa na Kondeboy bila Madam Rita,” Harmonize alisema.

Vilevile aliwarai vijana wote kutokata tama badala yake kuzidi kujituma maadamu wana kipaji na wanaamini kwamba siku moja watafanikiwa.

Kuna asilimia ya mashabiki waliokuwepo kwenye hafla hiyo ambao hawakupenda kitendo cha ‘Jeshi’ kumpigia Rita magoti ila baadhi pia walikubaliana nacho wakisema ilikuwa ishara nzuri ya kutoa shukurani.

Ikumbukwe kwamba wakati Harmonize anaanza safari yake ya muziki, madam Rita alimwambia kwamba hawezi katu kuimba na kumtaka atafute kazi nyingine ya kufanya.

Zaidi ya miaka mitano baadaye, Harmonize ni moja kati ya wasanii wakubwa ndani ya Bongo na Afrika Mashariki.

 

View Comments