In Summary

• Msanii kutoka Tanzania, Whozu amewaomba wanaume kuwaheshimu wanawake.

• "Mwanamke anajitoa mhanga sana, ikifikia hatua anakuzalia unapaswa kumheshimu sana," Whozu aliandika.

Instagram, KWA HISANI
Image: Whozu

Msanii kutoka Tanzania, Whozu amewaomba wanaume kuwaheshimu wanawake.

Alizungumza haya baada ya mkewe, Cappuccino Tunda  kujifungua mtoto.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Whozu alisema kwamba wanawake wanapitia changamoto nyingi wanapokuwa na mimba hadi pale wanapojifungua.

Alisema kwamba wanawake wana uwezo wa kuavya mimba kutumia P2  ila wanakubali kuvumilia uchungu wote ili kuleta viumbe duniani.

"Mwanamke anajitoa mhanga sana, ikifikia hatua anakuzalia unapaswa kumheshimu sana," Whozu aliandika.

Whozu alisema kwamba yupo tayari kupambana kivyovyote vile kuhakikisha kwamba mkewe na mnawe hawakosi chochote na wanaishi maisha mazuri.

Wasanii mbalimbali wakiwemo Nandy, na Wolper walimpongeza kwa kauli yake iliyoonyesha ukomavu wa akili.

"Umekua sana kijana," Nandy aliandika.

View Comments