In Summary

• Eric Omondi alipakia video akichoma kitambulisho chake cha kitaifa huku akiwataka Raila na Ruto kukutana naye chini ya siku tano kuzungumzia mikakati ya kuwaokoa vijana kutoka hali ngumu ya maisha.

Eric Omondi
Image: Instagram

Mchekeshaji Eric Omondi ameendelea kampeni zake za kuhamasisha vijana dhidi ya kuchagua viongozi wasiofaa katika uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.

Amezianza kampeni zake mitandaoni wiki hii kwa kufanya matukio mbalimbali ya kustaajabisha na kuchekesha kwa pamoja.

Juzi mchekeshaji huyo alitoa siku saba kwa farasi wakuu katika kinyang'anyiro cha urais cha mwaka huu, Raila Odinga na William Ruto. Omondi aliwataka wawili hao kumtafuta katika kipindi cha siku saba zifuatazo kwa ajili ya mazungumzo.

Siku moja baadae alipakia video kwenye mtandao wake wa Instagram akiwa amejifunga minyororo mwili mzima kwa kawaida yake ya kutovalia shati.

Katika video hiyo aliyoonekana akitembea katikati mwa jiji la Nairobi aliburura minyororo, Omondi alisema kwamba alikuwa anaonesha vijana ni jinsi gani walivyokuwa watumwa kwa nchi yao hali ya kuwa wao ndio wengi wenye kufanya uchaguzi wa busara debeni.

Alisema kwamba maisha ya vijana wengi yamefungwa katika minyororo na hakuna chochote wanaweza fanya kwa sababu ya kuwachagua viongozi wafisadi wanaojijali wenyewe.

Jumatano pia Omondi ameendeleza harakati zake ambapo amefanya jambo la hamaki mno alipoweka video akiwa anachoma kitambulisho chake cha kitaifa.

Katika video hii ya Jumatano, Omondi anaigiza muonekano wa ‘marasta’ ambapo amevalia kofia ya wigi la kirasta, na muziki aina ya Reggae wa msanii maarufu Lucky Dube unasikika ukiimba maudhui ya wafungwa wa utumwa.

Eric Omondi ameambatanisha ujumbe akisema kwamba kampeni hizi ni kuelekea kutamatika kwa makataa ya siku saba alizotoa kwa viongozi hao wa marengo mikuu nchini na kusema zimesalia siku tano tu na lazima watatii.

“Safari hii lazima watatusikiliza, iwe kwa moto au kwa kutumia nguvu. Siku 5 zimesalia na iwapo Raila na Ruto hawatatupatia mbinu bora ya kuimarisha maisha sisi kama vijana, basi hatutakuwa na budi ila kulazimika kuchukua maamuzi ya vitendo vikali dhidi yao,” aliandika Omondi.

Huyu bwana ni mwanaharakati mpya kabisa wa kila kitu kinachowahusu vijana, si muziki, si siasa, kila kitu!

View Comments