In Summary

•Nana Owiti alishukuru familia yake kwa upendo mkubwa ambao wamemwonyesha na jinsi ambavyo wameendelea kumuunga mkono.

•King Kaka alimsherehekea mkewe kama rafiki wake mkubwa, mshirika wake kweli na mama ya watoto wake

Image: INSTAGRAM// KING KAKA

Mtangazaji Nana Owiti ambaye ni mke wa rapa Kennedy Ombima almarufu King Kaka aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa mnamo Jumanne.

Bi Owiti alimshukuru Mola kwa yote aliyomtendea maishani. Vilevile alishukuru familia yake kwa upendo mkubwa ambao wamemwonyesha na jinsi ambavyo wameendelea kumuunga mkono.

"Safari nyingine ya kuzunguka jua . Nimebarikiwa sana. Nimejikusanyia nguvu nyingi, nimepata hekima nyingi, nimesherehekea upendo mwingi, nimejipamba kwa wema, nimezama katika subira, nimejifunika kwa upole na ukali. Hakika najitahidi kuwa msukumo bora kwa mdogo wangu na vizazi vijavyo. Namshukuru Mungu kwa yote makubwa, madogo na yaliyo katikati. Nashukuru familia yangu kwa upendo na jinsi ambavyo mmendelea kuniunga mkono. Siichukulii kawaida. Heri ya Siku ya Kuzaliwa kwa mkosoaji wangu mkubwa, mimi," Bi Owiti alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mamia ya wanamitandao wakiwemo watu mashuhuri walimtakia mama huyo wa watoto wawili kheri za siku ya kuzaliwa.

King Kaka kwa upande wake alimsherehekea mkewe kama rafiki wake mkubwa, mshirika wake kweli na mama ya watoto wake. Alitoa hakikisho kwamba angependa wazeeke pamoja.

"Leo ni siku ya kuzaliwa ya rafiki yangu wa dhati. Kienyeji yangu safiii. Mama wa watoto wangu, mwenzangu wa kweli, mke wangu, mtu wangu wa nguvu. Asante Nana Owiti kwa kuwa hapa kila wakati na kuwa wewe. Heri ya mwaka mpya!!! Hadi tukunje mgongo," King Kaka alisema.

Wawili hao wamekuwa pamoja kwa zaidi ya mwongo mmoja na wamebarikiwa na watoto wawili pamoja.

View Comments