In Summary

• Msanii Diamond Platnumz anasema ngoma ya Nawaza anaipenda kwa sababu ni aina ya ngoma ambazo zilimtoa.

Instagram, KWA HISANI
Image: Diamond Platinumz

Staa wa bongo fleva Diamond Platnumz anasema wimbo wake pendwa kabisa katika EP yake ya FOA si mwingine bali ni ule wa Nawaza na akatoa sababu nyingi tu kwa nini anaupenda kama watu wengine.

Akizungumza katika runinga ya Wasafi, Diamond alisema kwamba wimbo huo ndio aliouandika kwa muda mrefu zaidi na pia ni aina ya ngoma ambazo zilimtoa kimuziki enzi za kipindi anaanza.

Msanii huyo pia alitoa sababu za kutunga wimbo kama huo ambao umekubaliwa na wimbo licha ya kuwa si wa kuchangamka kama ambavyo wengi wanazoea.

“Katika EP yangu nazipenda nyimbo zote lakini nafikiri Nawaza naipenda sana. Na kwa nini naipenda Nawaza? Unajua wakati mwingine watu wanadhani sijui nimesahau kuandika muziki au nimeacha kuandika. Mimi nilizaliwa Mungu akanipa taanta ya kujua kuandika miziki ya kibongo fleva,” alisema Diamond.

Diamond pia alisema yeye anaandika miziki mingine ili iweze kuenda mbali na kufanya vizuri zaidi katika majukwaa na masoko mbalimbali.

Alikiri kwamba hii ndio ngoma ambayo aliketi chini na kuandika na akasema kwamba anajua imezua gumzo mitaani kwa baadhi ya vipengele, lakini pia akasema ukiandika ngoma halafu izungumziwe basi hiyo ndio bongo fleva.

“Nawaza is my favourite song na sio kama sijaandika nyimbo kama hizo kwa muda mrefu, ninazo lakini naona hii ndio best,” alisema Diamond.

Akionekana kuwajibu wanaozua gumza kuhusu kipande anachozungumzia clip za Rayvanny na Elizabeth, Diamond alisema utunzi wa mistari katika ngoma xake uko hivo na kwamba kuzungumziwa hivo ina maana ngoma hiyo imekubalika.

View Comments