In Summary

• Eddie Butita amesema  kwamba umaarufu wa wasanii huwezi kuwasaidia kushinda nafasi za uongozi .

• Amewataka wasanii hao kutoa manifesto zao ili wananchi wachague viongozi faafu.

Instagram, KWA HISANI
Image: Eddie Butita

Mcheshi Eddie Butita amefutilia mbali madai kwamba msanii anaweza kushinda uchaguzi kutokana na umaarufu wake.

Kupitia video iliyopakiwa katika  akaunti ya Youtube ya Spm Buzz, Butita alisema kwamba wasanii wanaojitosa siasani wanapaswa kuwasilisha sera zao wala sio kutumia umaarufu wao kuingia uongozini.

Butita alishikilia kwamba ustaa na uongozi ni mambo mawili tofauti, kwa hiyo wasanii hawapaswi kuingia kwenye kivumbi hicho wakidhani watashinda moja kwa moja.

"Sio kila staa atakuwa kiongozi mzuri, wengi hawana miradi waliyofanikisha'" Butita alisema.

Aliwataka wananchi kuwakagua kwa undani wasanii hao na kufahamu ajenda zao za maendeleo pindi watakapoingia mamlakani.

Aidha, alisema kwamba wasanii ambao wataibuka kidedea ni wale ambao tayari wameonyesha moyo wa kusaidia wananchi wa kawaida na kuboresha maisha yao.

Kauli hii ya Butita inajiri wakati ambapo wasanii wengi kama vile Jalang'o, Mc Jessy miongoni mwa wengine wamejitosa ulingoni kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

 

View Comments