In Summary

• Mwanablogu na msanii chipukia Diana Marua amesema kwamba hawezi akatoa msaada wa pesa kwa mashabiki wake.

• "Wewe ndo utaamua kama utakuwa unatazama kazi za wengine ama utaweka zako watu watazame," Marua alisema.

Instagram, KWA HISANI
Image: Diana Marua

Mwanablogu na msanii chipukia Diana Marua amesema kwamba hawezi akatoa msaada wa pesa kwa mashabiki wake.

Kauli hiyo ilijiri baada ya kupata jumbe nyingi za watu waliokuwa wakimuomba msaada wa hela ili kuendeleza maisha yao au hata kupata chakula cha kila siku.

Kupitia video aliyopakia katika akaunti yake ya Youtube, Diana aliwarai mashabiki wake kutumia simu zao kutengeneza 'content' , ambayo itawasaidia kupata hela ikifahamika kwamba tupo katika karne ya ishirini na moja [kizazi cha kidijitali].

Marua alisisitiza kwamba inaweza ikachukua muda kwa yeyote kuanza kupata hela mtandaoni, wale ambao tayari wameanza kujituma wana nafasi kubwa ya kufanikiwa.

"Wewe ndo utaamua kama utakuwa unatazama kazi za wengine ama utaweka zako watu watazame," Marua alisema.

Kwa muda sasa asilimia kubwa ya mashabiki hudhani kwamba mastaa hawapitii changamoto katika kudumisha mtindo wao wa kimaisha , jambo ambalo lilimpelekea Marua kuwapa mashabiki ushauri huo.

 

View Comments