In Summary
  • Kanze Dena alikuwa mwanahabari mwenza wa Lulu kabla ya kupata wadhifa wa msemaji wa ikulu
Lulu Hassan

Urafiki kati ya mwanahabari wa runinga ya Citizen Lulu Hassan na msemaji wa Ikulu Kane Dena umekuwa ukinoga kila kuchao.

Kanze Dena alikuwa mwanahabari mwenza wa Lulu kabla ya kupata wadhifa wa msemaji wa ikulu.

Huku Kanze akisherehekea siku yake ya kuzaliwa siku ya Jumanne wanamitandao walimtumia jumbe za kipekee alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Kwa upande wake Lulu alimwandikia ujumbe wa kipekee na kumtakia Mungu ampe hitaji la moyo wake.

"Happy Birthday dadaa mkubwa ,Mungu akupe hitaji la moyo wako ....❤❤ u dada mwenye roho yake @kanze_dena ..Uendelee kuwa baraka kwa wengi," Lulu Aliandika.

Mwanahabari huyo wa zamani wa Citizen TV alienda kwenye mitandao yake ya kijamii kusherehekea siku hii akisema anajivunia mwanamke ambaye amekuwa.

View Comments