In Summary

• Mchekeshaji huyo alipata umaarufu mkubwa wakati alifanya maigizo ya Wash Wash mwaka jana

Terence Creative na mkewe Milly Chebby
Image: Terence Creative//Facebook

Mchekeshaji na mujigizaji Terence Creative amesherehekea miaka kumi katika ndoa na mkewe Milly Chebby kwa kupakia picha mbali mbali zinazohadithia safari ndefu ya mwongo mmoja ya mapenzi yao yasiyojua kufa.

Terence aliibuka katika uwanja wa umaarufu mwaka jana baada ya kufanya maigizo ya Wash Wash ambapo alikuwa anaigiza kama mwanaume Mkongo ambaye ni Tajiri anayelaghai watu mali na pesa kwa kuwadanganya kuwa baada ya kuziosha zinaongezeka.

“Matamu na matungu ya ndoa. Imekuwa miaka 10 pamoja na bado tunaendelea,” aliandika Terence kwenye msururu wa picha hizo.

View Comments