In Summary
  • Akiongea kupitia insta stories , bintiye mwanasiasa huyo pia alifichua kwa nini bado yuko single

Binti mdogo zaidi wa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko, Sandra amewaeleza wafuasi wake kwa nini hana tattoo kwenye mwili wake.

Akiongea kupitia insta stories , bintiye mwanasiasa huyo pia alifichua kwa nini bado yuko single.

Sandra alifungua jukwaa lake la Instagram kwa maswali na majibu. Katika kipindi hiki, wanamtandao kadhaa walimuuliza maswali ya kibinafsi.

Sandra alielezea umma kwa nini hana tattoo kwenye mwili wake. , Thicky Sandra aliulizwa na shabiki ikiwa ana tattoo yoyote.

Alijibu kwa kusema:

'Hapana. Je, unaweza kuweka kibandiko kwenye Bentley'. Sandra alisema kwamba hawezi kujichora tatoo kwenye mwili wake.

Kwenye chapisho lililofuata, mtu mashuhuri alifichua kwa nini bado yuko single. Mtayarishaji mchanga wa maudhui alidai kuwa anataka kuwa peke yake kwa muda.

Thicky aliendelea na kuongeza kuwa haitaji mwanaume maishani mwake

View Comments