In Summary

• Irene Uwoya amewataka mashabiki wake kujituma kwa kile alikitaja kuwa umaskini unapotezea mtu heshima katika jamii.

• Kulingana naye unapokuwa na hela kuna mambo mengi ambayo unawezakuyafanya.

Irene Uwoya
Image: Ireneuwoya/INSTAGRAM

Mwanafilamu na mfanyibiashara kutoka Tanzania, Irene Uwoya amewataka mashabiki wake kupambana zaidi katika maisha kwani umaskini unadhalilisha.

Kupitia ujumbe ambao alichapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Uwoya alisema kwamba umaskini unamfanya mtu kukosa umuhimu na kudharauliwa katika jamii.

"Tupigane sana umaskini unadhalilisha sana," Uwoya aliandika.

Uwoya anafahamika kwa hulka yake ya kuishi maisha ya juu, ikionyesha kwamba anajituma kuhakikisha anadumisha kiwango hicho cha maisha.

Mashabiki nao walionekana kukubaliana naye kwa jinsi ambavyo amewamotisha kina dada wengi, kutokana na mitindo yake ya kimaisha.

"Nakuelewa na miondoko yako sana, swaga zako ni za kibabe," shabiki mmoja aliandika.

Wengine walisema kwamba ukiwa maskini hata wandani na wanafamilia hukosa kukuheshimu kwa kuwa huna la mno unalochangia.

Je wewe unakubaliana kwamba ukosefu wa hela unasababisha dharau katika jamii?

View Comments