In Summary

• Wahubiri hao ambao pia ni wanandoa wamedumu katika taasis ya ndoa kwa takribani miongo mitano sasa.

Mchungaji maarufu nchini Kenya JB Masinde na mkewe kutoka kanisa la Deliverence lililoko katika mtaa wa Umoja jijini Nairobi wamekuwa kwa mudqa mrefu wakitumiwa kama mfano hai wa mahusiano ya kimapenzi yaliyo bora.

Watumishi hao wa Mungu wamedumu katika ndoa kwa miaka 46 sasa na hawakawii kutoa ushauri na chanzo cha mahusiano yao kudumu kwa takribani miongo mitano sasa.

Katika moja ya video iliyopakiwa kwenye ukurasa wa kanisa hio wa Facebook, mkewe JB Masinde, Persia Masinde anaonekana akiwahutubia umati wa waumini na kuwadadavulia virutubishi vya kustawisha mahusiano ya ndoa ili kudumu kama yao.

“Mimi nawaombea nyinyi wote kwamba ndoa yenu isiwe moja ya takwimu za ndoa zilizovurugika. Mnajua siku hizi kuna misukosuko katika ndoa nyingi, lakini mimi nawashangaa hao, mbona wasitutizame sisi, miaka 46 na bado tunapendana,” alisema Persia Masinde.

Pia alifichua kwamba kudumu kwao katika ndoa haina maana kwamba hawana changamoto bali huwa zinawakabili na wao huzitatua pindi zinapokuja na kuzipotezea kabisa, huku akisema zana kubwac ya kulinda mahusiano ni kusameheana kwa sababu kila mmoja atakosea.

“Kitu kimoja ambacho hamfai kusahau ni kwamba ndoa muda wote ni kuhusu msamaha na haiwezi dumu kama hakuna kusameheana kwa sababu mtu atakuwa na haraka ya kukimbia lakini wakati mnasameheana mnaanza upya na safari ya mahusiano inaendelea,” mchungaji Persia alitoa ushauri.

Mchungaji huyo alisema ni mpango wa Mungu kuwepo kwa ndoa na haifai kuvunjika wakati wawili wanapopendana na kuamua kuwa mwili mmoja.

Wawili hao kwa kipindi hicho cha miaka 46 kwenye ndoa takatifu, wamebarikiwa na watoto wanne na wajukuu kumi na mmoja. Aliwataka wanandoa wachanga wakati wanahisi kuchoka na ndoa wawatazame wao na kupata motisha wa kuendeleakuwepo kwenye ndoa kwani ni kitu ambacho kinamfurahisha Mungu.

View Comments