In Summary

• Mueni Bahati alisema anatarajia watoto mapacha ambao wote watakuwa wa kike.

• Diana Marua alisema yeye hana shinda na mtoto yeyote ambaye Mungu atambariki naye.

Mwanamuziki Diana Marua na familia yake
Image: YouTube//screengrabs

Mwanamuziki wa kufoka na mkuza maudhui Diana Marua amepakia video kwenye YouTube yake akiwauliza watoto wake wanne kuhusu maoni yao ya yule mtoto ambaye wanatarajia, wiki mbili baada ya kuutangazia ulimwengu kwamba anatarajia mtoto mwingine.

Watoto hao wanaonekana kufurahia huku wakisema kwamba tangu aweke wazi kwamba ni mjamzito, watoto wake wamekuwa wakirudi kutoka shuleni kila jioni na kutarajia kupata mtoto huyo ameshazaliwa.

Morgan, ambaye ni mtoto Bahati alimpaka kutoka mitaani alikuwa wa kwanza kuulizwa iwapo angependa kijacho awe mtoto wa kike au wa kiume, ambapo kijana huyo mtanashati alisema bila kubabaika kwamba anatarajia mtoto atakayezaliwa awe ni anataka mtoto awe ndugu yake wa kiume.

“Mimi nataka awe wa kiume kwa sababu napenda tu wavulana,” alisema Morgan.

Alisema kwamba bado anampenda ndugu yake mdogo Majesty lakini pia anataka ndugu mwingine wa kiume.

Aliyeshangaza ni mueni ambaye ni mtoto ambaye Bahati alizaa na mwanamke mwingine kwa jina Yvette Obura ambaye alisema kwamba yeye hatarajii kitu chochote chini ya mapacha na kusema kwamba anatarajia wote wawe mapacha wa kike mpaka akaomba Mungu awape mapacha hao.

Mtoto wake wa kwanza kwa kumzaa, Heaven Bahati alisema kwa upande wake angependa kumuona ndugu wa kike kwani wa kiume wanachosha tu.

“Mimi nataka mtoto ambaye ataitwa Heaven kama mimi ndio niwe nikimbeba na pia kulala na yeye,” alisema mtoto huyo.

Watoto hao hatimaye walimuuliza kama anataka mtoto wa kike au wa kiume na Diana Marua aliwajibu kwamba yeye hana tatizo na mtoto yeyote ambaye Mungu atampa kwani atashukuru tu pakubwa.

View Comments