In Summary

• “Hakuna Wasanii matajiri Tanzania baada yangu, zaidi ya wale wa WCB. Nilifanya haya kwa kuwekeza mamilioni ya pesa zangu kwao" - Diamond.

Msanii Diamond Platnumz akiwa nac wasanii walioondoka WCB Wasafi, Harmonize, Rayvanny na Rich Mavoko
Image: Facebook

Kwa wiki kadhaa sasa tangu kuondoka kwa msanii Rayvanny kutoka lebo ya WCB Wasafi, kumekuwa na minong’ono mitandaoni huku watu wakiachia maoni kinzani kuhusu hali ilivyo katika lebo hiyo hadi kuwapelekea mastaa kuondoka na kuanzisha lebo zao.

Miaka mitatu iliyopita, palizuka na Sakata kama hilo ambapo msanii Harmonize aliondoka kwa njia ya kishari kabisa ambapo baadae alienda na kuzua dhana za kuilaumu lebo hiyo kwa unyonyaji wa mapato ya wasanii walioko chini yake. Harmonize alifichua kwamab mkataba wake aliopewa chini ya Wasafi ulikuwa unaruhusu lebo kuchukua asilimia 60 ya mapato na msanii kubakia na asilimia 40 tu.

Pia msanii huyo alidai kwamba aliipishwa zaidi ya milioni 600 pesa za benki kuu ya Tanzania ili kuuvunja mkataba wake, na pia kumlazimu kuchukua hatua za kumshtaki Diamond kwa rais kipindi hicho hayati Magufuli ili kuingilia kati kwa Harmonize kupata uhuru wake mbali na lebo ya Wasafi.

 

Kuondoka kwa Rayvanny pia hakukuwa kirahisi tu kwani msanii huyo alilazimika kulipa Shilingi Bilioni moja za Kitanzania ili kununua sehemu iliyobaki ya mkataba wake wa miaka 10, suala amablo limeibuqa mjadala ule ule tena kuhusu Lebo ya WCB Wasafi inavyowachukulia Wasanii wake.

Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen nchini humo, Mmiliki wa Lebo hiyo, Diamond Platnumz amesema haoni tatizo kuhusu mkataba huo ambao wengi wanadai kuwa ni mkataba wa ‘kinyonyaji’ ambao unaifanya WCB Wasafi kuchukua asilimia 60 ya mapato yote yanayotokana na kila Msanii aliyesajiliwa chini ya lebo hiyo.

“Tuweke kitu kimoja sawa, muziki ni biashara. Wanaolalamika tunawanyonya Wasanii wanaonekana kusahau Wasanii hawa walikuwa kwenye Lebo nyingine tofauti lakini hawakuwa maarufu. Tuliwachukua, na tukawatengeneza hadi wakafikia hatua ya kuuzika na kuzalisha pesa nzuri tofauti na ilivyokuwa hapo awali. WCB tuliwafanya kuwa matajiri na maarufu na unawasikia wanathibitisha" gazeti hilo linanukuu.

Diamond pia anazidi kutetea mkataba huo kwa kusema kwamba licha ya lebo kuchukua asilimia kubwa kuliko msanii lakini hakuna wasanii Tajiri zaidi nchini humo kuliko wasanii walioko au waliowahi kuwepo katika lebo ya WCB Wasafi.

“Hakuna Wasanii matajiri Tanzania baada yangu, zaidi ya wale wa WCB. Nilifanya haya kwa kuwekeza mamilioni ya pesa zangu kwao, lakini sasa msanii anapoanzishwa, anataka kukimbia na biashara nzima. Siwezi kuruhusu hilo, ilibidi nirudishiwe pesa zangu na faida pia" alinukuliwa Diamond.

Bosi wa lebo ya WCB Wasafi, Diamond Platnumz.
Image: Instagram//DiamondPlatnumz
View Comments