In Summary
  • Wakenya wa tabaka mbalimbali wameendelea kumtakia Bi Ida kheri ya siku ya kuzaliwa na kumuombea baraka maishani
Image: Raila JUnior/TWITTER

Huku mkewe kinara wa ODM Ida Odinga akisherehekea siku yake ya kuzaliwa amepoke jumbe nyingi kutoka kwa mashabiki na hata familia.

Mke huyo wa mgombea urais wa Azimio-One Kenya Raila Amollo Odinga anasherehekea kutimiza miaka 72.

Wakenya wa tabaka mbalimbali wameendelea kumtakia Bi Ida kheri ya siku ya kuzaliwa na kumuombea baraka maishani.

Mwanawe Ida,Raila Junior alimsherehekea mama yake kwa ujumbe wa kipekee na hata kumshukuru kwa kuwa mama yake.

Ida amekuwa akionekana akimuunga Riala mkono katika safari yake ya siasa.

Raila Junior aliandika;

"Nimebarikiwa sana kuwa na mwanamke kama wewe katika maisha yangu.Umenionyesha upendo mkuu na huruma kwa miaka yote na ninakushukuru sana kwa hilo.Heri ya Kuzaliwa kwako leo, mama."

 

View Comments