In Summary

• Alipoulizwa iwapo wanashirikiana katika kulea mtoto wao, Mwanamama huyo alikwepa swali na kusema kwamba hangependa kuingilia sana katika suala hilo.

• Pia alisema kwamab aliuza gari ambalo Diamond aliwahi kumpa kama zawadi enzi wakiwa wapenzi.

Diamond, Mobetto Mwanamitindo huyo alisema hajui ni kwa nini baba mtoto wake, Diamond Platnumz hakumtakila kila la kheri mtoto wao
Image: Instagram

Mwanamitindo na mjasiriamali kutokea Tanzania Hamisa Mobetto ameshindwa kuelewa ni kwa nini mzazi mwenziwe, msanii Diamond Platnumz hakumtakia kila la kheri mtoto wao licha ya kufahamu fika kwamba ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari za umbeya nchini humo, Mobetto alikuwa anajibu maswali mbali mbali kutoka kwa wakuza maudhui hao wa mitandaoni ambapo pia alidokeza kwamba kila mpenzi ambaye amekuwa naye huwa anampa zawadi ya gari.

Mama huyo wa watoto wawili kila mmoja na baba yake alidokeza kwamab baba za watoto wake wote wamewahi kumtunuku gari, akiwemo Diamond Platnumz ila akasema kwamab magari hayo aliyauza kitambo kutokana na za kibinafsi.

Alipoulizwa suala la Diamond, Mobetto alionekana kuruka na kukataa kabisa kulizungumzia suala lolote kuhusu msanii huyo nguli wa Bongo Fleva huku akiwataka waandishi hao badala yake kujua kutoka kwa Diamond ni kwa nini hakumtakia kila la kheri mwanao siku yake ya kuzaliwa, jambo ambalo hata yeye lilionekana kumfanya kukuna kichwa.

Suala la mtoto wake na Diamond ambaye ni wa kiume kutoshangiliwa na babake siku yake ya kuzaliwa lilizua mjadala mkali baada ya majasusi makini wa mitandaoni kubaini kwamba Diamond alisalia kimya muda wote watu kadhaa walipokuwa wakimtumia mtoto huyo jumbe za kumtakia kila la kheri.

“Kusema kweli sifahamu kwa nini Diamond hakumtakia kila la kheri mtoto. Nadhani hilo swali ni vizuri akiulizwa yeye mwenyewe binafsi. Mimi nitakuwa sina majibu na mimi si mtu ambaye ninapenda kuuliza, nadhani ni maamuzi tu, mtu unaamka asubuhi unaamua tu,” Mobetto alijibu huku akitolea mfano wa babake ambaye hakuwahi kumtakia kila la kheri siku yake ya kuzaliwa enzi hizo ambazo hazikuwa zimeuona mwanga wa mitandao ya kijamii.

Alipoulizwa kama wanashirikiana vizuri katika malezi ya mtoto, Mobetto alidinda kujibu hilo na kusema kwamba yeye hapendi kulizamia zaidi suala lolote linalomhusu Diamond na kusema kwamba jambo la kumtakia mtoto kila la kheri haliongezi wala kupunguza kitu chochote katika maisha ya mtoto wake.

View Comments