In Summary

• Juzi kati alisema katika mahojiano kwamba wanadada wengi wamefurika kwenye DM zake wengine wakitafuta umaarufu kupitia yeye na wengine pesa.

Msanii Stevo Simple Boy atokelezea na muonekano mpya
Image: Instagram

Ama kweli Mungu akiamua kukupa, anakupa kwa mkono wa kushoto tena tumbi nzima!

Msanii Stevo Simple Boy miezi kadhaa baada ya kufanyiwa madhira katika lebo ya awali ambapo ilisemekana anadhulumiwa kifedha na hata kuondoka kwake kukawa si kwa furaha baada ya lebo ile kupiga tanji akaunti zake za mitandaoni, msanii huyo sasa ametokelezea kwa muonekano mpya kabisa wa kutia naksi machoni pa wengi.

Msanii huyo baada ya kupoteza akaunti zote, alikumbatia msemo kwamba kuanza sifuri ni ujinga bali ujinga ni kuogopa kuanza, kwake yeye, alianza sifuri kwa kujijenga upya na kuingia katika lebo nyingine ambapo mafanikio yake yamejipa tena kwa njia kubwa ajabu kinyume na matarajio ya wengi.

 Baada ya kupakia picha hiyo inayomtoa kwa njia tofuati kabisa, Simple Boy sasa amewaaminisha wengi kwa maneno yake ailiyosema mapema wiki hii kwamba vipusa wengi wamefurika kweney akaunti zake za mitandao ya kijamii kumtaka wengine kuonekana naye, wengine kutaka hela na wengine kwa mapenzi.

Alipotoa madai hayo, wengi hawakumuamini ila sasa baada ya muonekano huo ni kweli huenda DM yake imefurika vipusa wanaomtolea midenda, hata licha ya kuweka wazi kwa umma shughuli yake ya kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake mpya Gee baada ya kutengana na Pritty Vishy ambaye alikuwa mpenzi wake wa muda mrefu.

Stevo alidokeza kwamba hivi karibuni atafunga harusi na Gee na katika picha hiyo yenye muonekano ndani ya suti alidokeza kitu kama shughuli kubwa kukaribia kufanyika ambapo wengi wanahisi huenda utakuwa ni muonekano wake wa siku ya harusi.

“Tayari tayari tarehe imefika,” Stevo Simple Boy aliandika na kuwaacha watu wakichanganua tarehe hii ya kufika yenye muonekano halisi wa kutia nakshi itakuwa ni ya tukio lipi!

View Comments