In Summary

• Azam alisema Diamond ndiye rais wa muziki wa bongo fleva hivyo atamlinda kwa nguvu na moyo wake wote, amesema ukitaka kumshambulia Diamond inabidi uanze na yeye kwanza.

ISSA AZAM, DIAMOND na ALIKIBA Chawa wa Diamond alisema kwamba yupo radhi kumukoa Diamond kutoka motoni na kuiacha familia yake
Image: Instagram

Chawa wa Diamond Platnumz ambaye ni kaka wa toka nitoke wa Alikiba, Issa Azam amefunguka kwamba ikitokea mke wake pamoja na Diamond Platnumz wote wamo motoni na yeye ndiye msaada wa karibu kutoa uokozi basi yupo radhi kumuokoa Diamond kwanza na mkewe baadae.

 

 Katika klipu fupi ambayo imezua mjadala mkali kwa kile wengi wanasema anahangaika juu chini kulazimisha undugu ka Diamond kisa bifu lake na kakake, Alikiba, Azam anaonekana akizungumza kwa kinywa kipana tena bila haya kwamba atamuokoa Diamond na kumkimbiza hospitali huku akimuacha mkewe.

 

Kulingana na yeye, Diamond ndiye mtu ambaye amemheshimisha kwa jina na mali yote anayomiliki na kwa hivyo ana kazi kubwa ya kulipa fadhila kwake kwa njia yoyote ile na kudai kwamba ako tayari kuacha mkewe ateketee kwa sababu wanawake ni wengi tena wapo ila kumpata mtu kama Diamond ni nadra kama kumpata mwanasiasa aliye mwaminifu.

 

Amefunguka zaidi kwamba Wanawake hawawezi kukuheshimu kama huna hela, hivyo ni sawa kumuokoa Diamond, kwani anampa hela pamoja na Umaarufu ambao unasababisha aweze kuhudumia familia yake.

 

Katika klipu nyingine ambayo pia ilizua mjadala sawa na huo, Issa alinukuliwa akikiri kwamba ikatokea kaka yake ambaye ni Alikiba wamejikuta motoni pamoja na msanii Diamond Platnumz, basi atamuokoa Diamond na kumuacha Alikiba ateketee kabisa.

 

Alizidi kumpamba Diamond kwa koja la maua na kusema kwamba msanii huyo ameokoa watu wengi sana ambao idadi yao haiwezi kukadiriwa na vikokotoo vya dunia hii na kumtamkia dua njema kwa Mungu azidi kumuweka hai ili azidi kuwarahisishia maisha wengine.

 

Azam alisema Diamond ndiye rais wa muziki wa bongo fleva hivyo atamlinda kwa nguvu na moyo wake wote, amesema ukitaka kumshambulia Diamond inabidi uanze na yeye kwanza.

 

Mbali na waliomponda pia kuna watu wameungana nae na wamesema ni sawa yeye kuongea hivyo maana Diamond anamsaada mkubwa kwake.

Awali aliwahi nukuliwa akisema kwamba walitengana na kakake Alikiba wakati alitaka kumtuma kumshambulia Diamond kwa mawe katika hafla moja ya tafrija ila akaghairi fikira zake na badala yake akaanza kumtetea Diamond.

View Comments