In Summary

• Mchungaji huyo pia aliitaka mamlaka ya KRA kuchunguza maisha ya wahubiri wanaoishi ya kifahari kumbe ni kwa pesa zinazotolewa kusukuma injili mbele.

Mchungaji Tony Kiamha kutoka kanisa la River of God amesema kwamba si kila sadaka wachungaji wanafaa kupokea kutoka kwa kila mtu.

Kiamah amewaambia wanaume wanaofanya usherati na uzinzi kwamba sadaka yao haifai kupokelewa kanisani na kuwataka wakwende nayo mbali kabisa na sehemu takatifu ya kuabudu.

Katika video ambayo mchungaji Kiamah aliipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram Jumanne, alikuwa akitoa funzo kwamba wanaume wa aina hiyo wanaofanya visa visivyompendeza Mungu na kisha kujinadhifisha kuelekea kanisani sadaka yao haihitajiki kabisa na wala wasijisumbue kutoa.

“Unakuja kanisani umepiga mke, unalala huku na kule na wake za wenyewe, na huku mkewe analia halafu unajifanya kuleta sadaka nono kanisani, Kwenda nayo, riswa! Pepo mbaya,” mchungaji Kuria anafoka kwa hasira.

Kwingineko pia mchungaji huyo aliwasuta wachungaji wanaoishi maisha ya kifahari kupitia pesa za kanisa na kuitaka mamlaka ya utozaji ushuru KRA kuwafanyia uchunguzi wa mali hizo.

“Ninatoa changamoto kwa KRA kuanza kanisani kwa sababu pesa zinazotolewa na wapendwa hawa waaminifu ni kwa ajili ya kuendeleza injili, na kusimamisha ufalme wa Mungu duniani. Kwa hivyo ikiwa pesa hizo hazitumiki kwa hilo, ni matumizi mabaya ya ofisi, na ni uhalifu,” Mchungaji huyo alinukuliwa.

KRA hivi karibuni ilitangaza kwamba itaanzisha mchakato wa kufuatilia maisha ya watu mitandaoni ili kubainisha mitindo na mifumo yao ya maisha ya kuwatoza ushuru ifaavyo.

View Comments