In Summary

• "Nitarudi baada ya kujikusanya na kupona. Mbona unacheat?” Cartoon Comedian aliuliza kwa hisia za uchungu.

Mchekeshaji Cartoon Comedian asemqa alisalitiwa kimapenzi
Image: Instagram

Mchekeshaji wa kike nchini Kenya, Cartoon Comedian baada ya muda mrefu kudokeza usumbufu katika mahusiano yake, hatimaye ameweka wazi kuhusu kile amabcho mashabiki wake wamekuwa wakifikiria.

Kupitia Instagram yake, Cartoon Comedian ameweka wazi kwamba aliyekuwa mpenzi wake alimsaliti kimapenzi kwa kuchepuka na kwa muda sasa amekuwa akijitahidi kukaa ngumu lakini imeshindikana.

Comedian alisema kwamba baada ya kugundua kuwa mpenzi wake alichepuka, alijaribu kujikaza ili kukaa kawaida watu wasijue lakini maji yamemfika shingoni na sasa ameamua kutema nyongo ili angalau aifungue nafsi yake.

Aliwaambia mashabiki wake kwamba amegundua yeye ni mtoto wa kike ambaye ni mdhaifu asiyeweza kujikaza na kuvumilia na kusema atachukua likizo mpaka pale atakapopona kutokana na kisa hicho kilichomtokea.

“Nimekuwa nikiumia kidogo, baada ya sakata la kuvunjika kwa mahusiano yangu ya kimapenzi. Nilifikiria mimi nitakaa mgumu kama Taliban lakini nimegundua mimi ni mtoto wa kike mdahifu. Nitarudi baada ya kujikusanya na kupona. Mbona unacheat?” Cartoon Comedian aliuliza kwa hisia za uchungu.

Itakumbukwa wiki chache zilizopita mchekeshaji huyo alidokeza kuachwa kupitia ukurasa wake wa Instagram ila wengi wakafikiria ni utani wake wa kawaida.

“Mtajuaje nimeachwa? Nikianza kumeremeta. Ukiona msichana anaparara, huyo ako katika mahusiano. Tukitoka kwenye mahusiano, tunaglow," mchekeshaji huyo alidai.

View Comments