In Summary

•Noah alisema "amefajika sana na safari yake" lakini kuna "sehemu nyingine ya maisha yangu ambayo ninataka kuendelea kuyaangazia".

•Alisema muda wa kuondoka kwake utatangazwa baadaye na kwamba ataendelea kutangaza kwa wakati huu.

Trevor Noah
Image: BBC

Mchekeshaji mwenye asili ya Afrika kusini Trevor Noah ametangaza kujiondoa kama mtangazaji wa kipindi cha The Daily Show cha nchini Marekani.

Noah alisema "amefajika sana na safari yake" lakini kuna "sehemu nyingine ya maisha yangu ambayo ninataka kuendelea kuyaangazia".

Mchekeshaji huyo mwenye umri wa miaka 38 amekuwa akiendesha kipindi cha habari za vichekesho na mazungumzo tangu kuchukua nafasi ya Jon Stewart mnamo 2015.

Alisema muda wa kuondoka kwake utatangazwa baadaye na kwamba ataendelea kutangaza kwa wakati huu.

Noah alianza uchezaji wake katika nchi yake ya asili ya Afrika Kusini, akitoa mifululizo ya vipindi maalum na kuandaa kipindi cha usiku kabla ya kuhamia Marekani mnamo 2011.

Bado alikuwa ni mtu asiyejulikana alipochaguliwa kuchukua kipindi cha Daily Show kwenye mtandao wa Comedy Central, lakini tangu wakati huo amekuwa nyota anayetambulika kimataifa na kushinda tuzo nyingi za televisheni.

Noah alitoa tangazo hilo mwishoni mwa kipindi chake cha Alhamisi usiku, na kusababisha mishtuko kutoka kwa watazamaji wa studio. “Nakumbuka tulipoanza... watu wengi sana hawakutuamini,” alisema.

"[Kuniteua kama mtangazaji] ilikuwa dau la kichaa kufanya. Bado jambo la wazimu kufanywa, na nafikiri bado ni chaguo la wazimu Mwafrika huyu wa kubahatisha.

"Ninashukuru kwa ajili ya safari hii. Imekuwa ya kushangaza kabisa. Ni kitu ambacho sikuwahi kutarajia."

View Comments