In Summary

• Akothee anakadiria kufunga pingu za maisha hivi karibuni na mpenzi wake kutoka Uswizi.

• Mwimbaji huyu amethihirisha kwamba amezamia kwenye bahari ya huba baada ya kupatana na mbavu yake.

Mwimbaji Akothee na mpenzi wake Bw Schweizer
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Asubuhi ya kuamkia Jumatano mwanamuziki na Mjasiriamali Esther Akoth almaarufu Akothee amevuma mitandaoni baada ya kupakia picha ya mpenzi wake mpya akimwandalia chakula cha asubuhi chenye asili ya Uswizi.

Kulingana na Akothee mpenzi wake ambaye wanakadiria kufunga pingu za maisha hivi karibuni, mpenzi wake anaonekana akionyesha weledi wake kuandaa mkate katika tamaduni ya kwao Uswizi.

Mama huyu akizungumza kwenye ukurasa wake wa Facebook, alionekana mwenye bashasha na shukrani sufufu kwa mpenziwe kwa kumwandalia mkate huo wala sio Chapati.

''Mahabuba wangu alituandalia mkate wa Uswizi, auuu. Sikujua  pia anajua kutengeneza mkate na sio chapati tu.'' Akothe alisema.

Mama huyo wa watoto watano alikuli atajifunza kuoka mikate pia.

Mjasiriamali huyu aligeuka gumzo la siku mitandaoni alipotangaza mpenzi wake mpya baada ya kuchumbiana na wanaume 2 hapo mwanzo.

Lakini kwa sasa  anasema anaishi Paradiso kumpata Mswizi anayempenda.

Ingawaje anahofia kumtambulisha mpenzi wake mpya kwa Familia yake akisema kuna uwezekano mamake hatamkubalia kwani hapendi watu wanao ruka kwenye ndoa moja hadi nyingine.

Akothee alionekana baadaye akituma ombi kwa mamake akimrai kumwitikia mpenzi wake Bwana Schweizer kwani sasa anajawa na raha isiyo kifani na  amezamia kwenye bahari ya huba.

View Comments