In Summary

• Madini Classic alisema kuwa hakutaka kushiriki vita vya maneno naye kwa sababu alijua yeye ni mtoto wa kike.

Madini amsherehekea Vishy siku yake ya kuzaliwa kwa ujumbe wa kejeli
Image: Instagram

Wiki moja iliyopita katika mazungumzo ya Q&A kwenye ukurasa wake wa Instagram, mwanadada Pritty Vishy alifunguka kuwa yeye na msanii Madini Classic si wapenzi tena.

Vishy alikuwa anajibu swali la shabiki mmoja aliyetaka kujua mahusiano yao yanaendelea na hivyo Vishy akasema kuwa walishaachana kitambo na wala hawako pamoja tena.

Jibu hili lilipasua mitandao ya kijamii huku wengine wakitaka kujua kiini cha kuvunjika kwa mahusiano yake mapya miezi michache tu baada ya kuyaweka wazi, ambapo Vishy alisema kuwa yeye uvumilivu na kuwa mwanamke mtiifu katika ndoa ndicho kitu ambacho hakikuumbwa katika damu yake.

Jumatatu alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, wengi walisubiri kuona ni nini Madini Classic atafanya au kumpa zawadi ama kumtamkia ujumbe wa kumtakia heri njema.

Na kweli Madini Classic kwa mara ya kwanza alizungumzia suala hilo la kuachana na Vishy ambapo alimzungumzia moja kwa moja kuwa aliona madai hayo na kwamba aliamua kujinyamazia kiume kwa sababu hakuwa anataka kuchagua mkondo wa vita vya maneno mitandaoni kama ambavyo Vishy walipelekana na aliyekuwa mpenzi wake wa awali Stevo Simple Boy.

“Habari PURITY RODENYI siku chache zilizopita niliona majibu yako kwa shabiki aliyeuliza tuko pamoja mmmm!!!, ningefanya vurugu mara kwa mara lakini nikaacha tu,” Madini Classic aliandika huku akimtakia heri njema ya kuzaliwa.

Msanii huyo alizidi kuelezea sababu zake za kutochagua mkondo wa vita vya maneno kwa kusema kwamba Vishy ni mtoto wa kike na anahitaji kudekezwa kama mtoto.

“Wewe ni baby girl unahitaji kubembelezwa kama mtoto. Anyway HAPPY BIRTHDAY TO YOU @prittyvishy,” Madini Classic aliandika.

View Comments