In Summary

• Kwa uwezo wangu mdogo kiuchumi, na huu Umasikini wangu, nimemnunulia Zawadi ndogo ya Gari Dogo - Manara.

Wiki mbili zilipozipa, msemaji wa soka nchini Tanzania Haji Manara Sunday aliweka wazi kuoa mke mwingine baada ya kukorofishana na mke wa kwanza.

Manara kama hillo halijatosha kwa mara nyingine tena amezua gumzo mitandaoni baada ya Jumatano jioni kupakia video kwenye Instagram yake akieleza kuwa baada ya kumwacha mke wake wa kwanza, hakumuacha kwa njia ya kizembe bali kwa zawadi moja ya kukumbuka mahusiano yao ya awali.

Katika video hiyo, Marana anaonekana akimkabidhi mkewe wa kwanza zawadi ya gari na kufiatisha maelezo marefu kuwa kwa ustaarabu wa kwao, ukishamwacha aliyekuwa mkeo basi hupaswi kujenga chuki bali kumwachia kitu angalau kama kitoka unyumba.

Samahani sana mke wangu Ruby🙏🏻❣ Kwa Mila na Desturi zetu Mashomvi wa Pwani , hususan Pwani ya huku kwetu Mashariki mwa bahari ya Hindi, hutuwajibisha kutoa kitoka Unyumba Kwa Mkeo,pindi umuoleapo Mke mwingine,” alisema Manara.

“Nami Kwa uwezo wangu mdogo kiuchumi, na huu Umasikini wangu, nimemnunulia Zawadi ndogo ya Gari Dogo, Mke wangu mkubwa Rubainah, kama KITOKA UNYUMBA, walau impoze machungu ya kumletea mwenzie,” aliongeza.

Aliweka wazi kuwa tukio hilo lilifanyika nyumbani kwake na kusema kwamba baada ya kumkabidhi gari hilo, mkewe alikubali na kuufungua moyo wake kumpokea mke mwenza.

Manara ni msemaji wa muda mrefu wa maswala ya spoti nchini Tanzania. Aliwahi kuwa msemaji wa klabu ya Simba kabla ya kuwaasi na kujiunga na watani wao wa jadi, Yanga ambapo pia alikuwa msemaji kwa msimu mmoja kabla ya shirikisho la soka Tanzania TFF  kumpiga kwa kifaa kizito kichwani kwa kumpiga marufuku dhidi ya kujihusisha na masuala yoyote ya kispoti kutokana na matamshi ya kizembe dhidi ya watu fulani.

View Comments