In Summary

• Katika kitengo cha Best African Act, Zuchu atamenyana na mastaa kama Musa Keys, Ayra Starr, Burna Boy miongoni mwa wengine.

Romy Jons amtania Zuchu kuhusu kuteuliwa MTV
Image: Instagram

Romy Jons ambaye ni mcheza santuri na kaka wa msanii Diamond Platnumz katika siku za hivi karibuni ameonekana akichagiza utani wake dhidi ya msanii Zuchu, haswa akitilia chumvi suala la Zuchu kusemekana kutoka kimapenzi na kakake Diamond.

Jumatano alasiri msanii Zuchu aliweka wazi kuwa hatimaye ameteuliwa kuwania tuzo za MTV EMA katika kitengo kimoja na magwiji kama Burna Boy na wengine.

Baada ya kuweka wazi habari hizo, mastaa mbali mbali ndani na nje ya Bongo walifurika kwenye ukurasa wake na kumhongera huku wakisema kwamba kwa hatua ya kuteuliwa tu tayari yeye ni mshindi.

“Unstahili dada, nii tu taayri wewe ni mshindi Allah akuongoze..” Wema Sepetu alimpongeza.

Baba yake katika Sanaa ya muziki Diamond Platnumz pia hakuachwa nyuma kwani alifika pale na kumhongera kwa kuandika mistari ya ngoma yake mpya ya Kwikwi.

"Rakata Rakata rakata, Rekete reketee reketee, Rikiti rikiti rikitii... Rukutu Rukuutu" Diamond aliandika huku pia akipeleka kwenye Instastories zake kuwataka watu kuona kile ambacho yeye ameona kwa Zuchu na kumuunga mkono katika kuhakikisha tuzo hiyo imeletwa nyumbani.

Huku mastaa hao wakilichukulia kwa uzingatifu mkubwa kumpongeza, Romy Jons aliendeleza utani wake kwa kumwambia Zuchu kwamba hakuna kitu pale, akionesha kwamba huenda ataambulia patupu.

“Hakuna kitu hapo,” Romy Jons alimtania Zuchu.

Ikumbukwe hii si mara ya kwanza kwani wiki jana wakati Zuchu alipakia picha yake, DJ huyo rasmi wa msanii Diamond pia alimtania kwa kumwambia kwamba kakake hawezi mpenda kwani anavyomjua Diamond ni mtu wa kumezea mate watu wenye maumbo makubwa akitolea mfano mwanamitindo Zari Hassan.

Watu mbali mbali walimsuta vikali kwa kumwambia kwamba haoni jema katika shemeji yake.

wewe nawe hauonangi kitu positive na Shemeji yako? Bure kabisa nkt. Ningekuwea Zuchu wewe na dadako Esma mngekula block, mna roho nyeusi sana” Sean Betsy alimwambia.

“kuwa positive kwa sisi mashabiki wenu. Unavyosema hivo una dissapoint hata kwenye voting zetu.. UNAVYOSEMA HAMNA KITU!! STUPID BOY,” mwingine kwa jina Senene Watamu alimkandia.

View Comments