In Summary

•Walionekana wenye furaha kumbeba na kumkumbatia Shiru huku Nyakio akifunzwa jinsi  ya kushika mtoto mchanga.

•"Mabinti wamemkaribisha mdogo wao kwa furaha na bashasha, lakini watabadilisha nepi watajua," Nameless alisema kwa matani

Mabinti wa Nameless; Tumiso, Nyakio na Shiru.
Image: FACEBOOK// NAMELESS

Mwanamuziki Nameless amezungumza baada ya mabinti wake wa kwanza wawili kuenda kumuona dada yao mdogo kwa mara ya kwanza.

Mabinti hao, Tumiso na Nyakio walimtembelea mama yao Wahu Kagwi hospitalini baada ya kujifungua mtoto wake wa tatu. 

Walionekana wenye furaha kumbeba na kumkumbatia Shiru huku Nyakio akifunzwa jinsi  ya kushika mtoto mchanga.

Nameless alisema kuwa amefurahi kuwa baba ya mabinti watatu sasa na alifurahia upendo wa kindugu uliomo baina ya watoto wake.

"Mabinti wamemkaribisha mdogo wao kwa furaha na bashasha, lakini watabadilisha nepi watajua," Nameless alisema kwa matani.

Mabinti hao walionekana kuwa na wakati mwema na dada yao na kumthamini dada yao mdogo kwa kumbeba.

Siku chache zilizopita,kabla ya kumkaribisha kitinda mimba wao, Nameless alikuwa amesema kuwa mkubwa wa mabinti wake Tumiso,ako tayari kuwaongoza wadogo wake.

Alisema kuwa Tumiso alikuwa amejiandaa vizuri na kujitayarisha kumpokea Shiru hata kabla ya kuzaliwa.

"Binti wangu wa kwanza anatazamia kukutana na dada yake mdogo na ameonyesha kuwa ako tayari kuwaongoza kwa bidii na kuwa mfano mwema kwao,"mwanamuziki huyo alimsifia binti yake wa kwanza.

Nameless alisema kuwa kufikia sasa Tumiso amekuwa dada na mtoto mzuri mwenye nidhamu kwake na kuwa amemfanya ajivunie kuwa baba yake.

Wakati huo huo mwanamuziki huyo alisema kuwa binti yake wa kati Nyakio amejifunza mengi kutoka kwa dada yake Tumiso.

Alisema kuwa Nyakio sasa atapata mafunzo kutoka kwa Tumiso na kuwa mfano kwa dada yake mdogo, Shiru kwa wakati mmoja.

Nameless alisema kuwa watoto wake ni furaha yake ya moyo hata wawe wadogo kiasi gani na kuwa alifurahi kuwa na wakati kama huo na watoto wkae.

Alisema pia kuwa yeye na Wahu wako tayari kuwalea watoto wao.

View Comments