In Summary

• Alipakia picha moja iliyoeleza hisia zake huku akiutoa mwezi huu wa Oktoba kwa minajili ya kuwatambua wanawake waliokuwa na uja uzito uliowaharibikia na watoto waliofariki.

Brendah Jons
Image: Brendah Jons/INSTAGRAM

Mwanaharakati wa kupinga vitendo vya ubakaji Brenda Jons amewaonyesha upendo wanawake ambao walipoteza uja uzito wao ama watoto wao kufariki.

Jons aliangazia wanawake ambao wamepata changamoto kwa kupata ujauzito, ambao watoto wao walifariki baada ya kujifungua na wale ambao uja uzito wao uliharibika na kuupoteza.

Alipakia picha moja iliyoeleza hisia zake huku akiutoa mwezi huu wa Oktoba kwa minajili ya kuwatambua wanawake waliokuwa na uja uzito uliowaharibikia na watoto waliofariki.

Aliwaambia wanawake hao kuwa anawaelewa na walichokipitia hakijasahaulika na mtu ili waweze kuwa na matumaini ya mbeleni.

Aliongeza kuwa watoto ni zawadi ambayo haistahili kusahaulika na kuwa hao waliofariki wanafaa kukumbukwa.

"Kwa wale ambao wamekuwa na shida ya kupata watoto, tunawakumbuka. Wale ambao wana ujauzito baada ya kumpoteza mwengine, tunajua kuwa bado mmebeba hisia hizo za huzuni na kuwa bado mnawafikiria," Jons alisema kupitia picha hiyo.

Mwanadada huyo pia aliwahimiza wanawake hao kujivunia kuwa mama ya watoto hao waliopoteza.

Aliwaambia wanawake hao ambao huvalia tabasamu ili kuficha hali yao ya huzuni kwa kupitia hali ya kupoteza mtoto kuwa hisia zao zinazingatiwa na kuwa wasihisi kuwa peke yao.

"Kwa wale ambao bado mmeshikilia watoto wenu kwa roho zenu, tunajua kuwa bado mtaendelea kujiuliza kuwa kama bado wangekuwa nanyi wangekuwa vipi. Wacha mwezi huu uwe wa kujivunia kuwa na watoto mbinguni na pia kuonyesha upendo wetu kwao," Jons alisema kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Baadhi ya wanawake maarufu waliopoteza uja uzito wao ama watoto wao kufariki ni:

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Kambua - Alimpoteza mwanawe siku chache baada ya kujifungua.

Size 8 - Uja uzito wake uliharibika na kumpoteza mwanawe aliyekuwa akitarajiwa.

Nadia Mukami  alipoteza uja uzito wake wa kwanza.

Nusra Yusuf, mchekeshaji wa Churchill ambaye pia walitangaza miezi michache iliyopita kupoteza ujauzito wao na mpenzi wake.

View Comments