In Summary

• Willy Paul alijizawidi gari hilo la aina ya Mercedes Benz kwa video aliyopakia  kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Willy Paul

Mwanamtandao mmoja alitoa maoni yake baada ya Willy Paul kujizawidi gari aina ya Mercedes Benz na nambari ya usajili kuonekana kuwa ya 666.

Nambari hiyo iliyokuwa kwenye gari la Willy Paul ilisemekana kuwa nambari ya wanachama wa Illuminati.

Suala hilo lilizua gumzo mtandaoni baada ya Willy Paul kufichua gari hilo na kupakia video yake mtandaoni.

Mwanamtandao huyo alizungumzia jinsi watu wa Afrika huwa na fikira za kuonea gere mafanikio ya watu.

"Huku Afrika ukiwa maskini, ni kazi ya Mungu, ukiwa tajiri unaabudu mashetani, kwa hivyo ni Mungu yupi huyo anayetaka waja wake wawe maskini hohehahe?" Craig Cutler aliuliza .

Wanamitandao wengine walizidi kumtetea mwanamuziki huyo na kumpongeza kwa bidii yake iliyomfikisha alipo sasa.

"Tumekuwa tukimwona akifanya bidii kutoka zamani. Muache kuchapisha mambo mkiwakejeli watu ili kupata likes," Khatenje Esipila aliongeza maoni yake.

Willy Paul aligeuka gumzo baada ya kupakia video ya gari lake jipya la rangi ya manjano katika mtandao wake wa Instagram.

Aliwashukuru mashabiki wake kwa kumuunga mkono na kusema kuwa ni ukarimu wao ndio uliomfikisha alipo sasa.

Alisema kuwa mashabiki wake walimpa nafasi ya pili ili kujitambulisha kama msanii anayefanya kazi yake kwa bidii.

Aliongeza kuwa alijituza gari hilo kwa kazi ya kupendeza aliyohisi amekuwa akifanya kwa muda sasa.

"Mungu ametenda tena !!Asante Mungu kwa tuzo hii nyingine. Nimejituza kwa kufanya kazi murwa, nitaendelea vivyo hivyo," Willy Paul aliandika .

Hii ni baada ya wiki chache zilizopita mwanamuziki huyo kujizawidi matatu ambayo wengi walimkejeli kwa kusema kuwa anapaswa kuwa na gari inayostahili jina lake.

View Comments