In Summary

• Sasa najitangaza kuwa rais wa wanawake wote wasioolewa - Mugoh alisema.

• Mugoh alivishwa pete ya uchumba Julai mwaka huu na afisa wa jeshi la KDF.

Mpelelezi Jane Mugoh katika picha zake awali
Image: facebook

Mpelelezi mkuu wa kibinafsi Jane Mugoh ametangaza kuvunja mahusiano yake na mpenzi wake afisa wa jeshi la KDF miezi mitatu tu tangu kutangaza kuoana naye.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mugoh alisema kwamba tabia ya kuchepuka na kuwa na wanawake wengi ni baadhi ya masuala ambayo yalimsababisha kumaliza uhusiano wake na afisa huyo wa KDF.

Muggoh alisema kwamba hakuwa anajua tabia ya mpenzi wake huyo mpaka pale alipopakia picha zao pamoja kwenye mitandao ya kijamii na hapo ndipo alipatana na picha kutoka kwa wanawake wengi wakimtumia kumueleza kwamab afisa huyo hakuwa mtu mwaminifu kwani alikuwa amewatongoza wengi wa hao waliontahadharisha Mugoh.

“Nilipochapisha kuhusu uchumba wangu Julai, nilipokea jumbe za pongezi kutoka kwa wafuasi wangu, maadui kutoka mipasho ya vyombo vya habari, familia na marafiki. Heshima kubwa kwenu nyote. Siku hiyo hiyo nilipokea picha katika Dm (sms zinazosumbua) kutoka kwa wanawake wane. Wote walikuwa na uchungu kwa sababu huyu jamaa alikuwa amewachezea mtandaoni na kuwaahidi ndoa, ukweli alikuwa nje ya Kenya,” Mugoh alianza kuelezea katika chapisho hilo refu.

Alisema kwamba licha ya kupokea tahadhari hizo, bado alijipa moyo kwamba mpenzi wake angebadilika na kuachana na mambo ya kudanga na wanawake wengi, lakini hili halikubalidika kwani hata mama mkwe wake alimuelezea kinagaubaga kwamba mtoto wake hajabadilika tabia ya kuchepuka.

“Ninachagua kuwapuuza kwa sababu niliazimia kuifanya ndoa yangu isimame. Mwezi huu alirejea nchini. Marafiki zake wa shule, majirani, mama (mama mkwe wangu) walinithibitishia kuwa hajabadilika. Kwangu mimi sio juu ya furaha yangu, lakini huwezi kumuumiza mama yako mwenyewe, wanawake wa zamani, watoto wa damu, uongo kuhusu kazi, unanichukulia kama malkia huku kando kuna mwanamke analia na isipokuwa kuishi naheshimu mioyo. Nina heshima,” Mugoh alidhihirisha kukata tamaa alipoambiwa taarifa hizo.

Alisema kwamba kutokana na kupashwa habari hizo, aliamua kuchukua maamuzi magumu na kuanza safari ya matumaini – kuvunjilia mbali uchumba wake na afisa huyo.

Alisema kwamba hivi karibuni atarudisha kila kitu ambacho afisa huyo alimpokeza vikiwemo pete ya uchumba na zawadi zote alizompa. Pia aliweka wazi kwamba yupo singo na wala hatafuti mpenzi kwa sasa.

“Ninathibitisha kuwa #SINGLE , bize, mwenye furaha na wala sitafuti mpenzi, Ninarudisha pete na zawadi zote kwa mwenyewe. Haifai kupigana. Sasa najitangaza kuwa rais wa wanawake wote wasioolewa😂😂😂. Nawapenda nyote. Wapelelezi pia ni binadamu. Acha kuigiza kama malaika. Ninafurahi kwa maamuzi yangu yenye nguvu hata ingawa ni ya uchungu,” Mugoh alisema.

View Comments