In Summary

•  Mdee na Rotimi walifichua taarifa hiyo kisha kutangaza kuwa mtoto wanayetarajia ni wa kike.

Venessa Mdee na Rotimi
Image: Instagram

Mwanamuziki Vanessa Mdee na mchumba wake Rotimi wametangaza kutarajia mtoto wa pili.

Wachumba hao walifichua taarifa hiyo kisha kutangaza kuwa mtoto wanayetarajia ni wa kike.

" Tunatarajia mtoto wa pili..🙏🏽🎊✨UTUKUFU KWA MUNGU ... ni wa kike 💕,"  Mdee alisema.

Watakuwa na watoto wawili sasa baada ya mtoto wao wa kiume ambaye  walimkaribisha duniani mwaka jana.

Mashabiki wao wakiwemo watu wengine maarufu waliwapongeza wachumba hao.

"Hongera mpenzi,"hassansarah alisema.

"Awwww Vane furaha iliyoko usoni mwako. Hongera mpenzi wangu. Hongera sana kwako na familia yako inayoongezeka 💖💙,"talliaoyando aliandika.

"Yayyyyy ❤️❤️❤️Nyinyi mmebarikiwa na mmependelewa sana. Mungu aendelee kukuonyesha jinsi anavyokupenda 😊😊😊,"lilianmbabazi alisema.

Mdee na Rotimi wamekuwa wakichumbiana kwa muda sasa na walibarikiwa na mtoto mmmoja ambaye alifikisha mwaka mmoja Septemba 29, mwaka huu.

Miezi michache baada ya kumpata mtoto wao, Rotimi  alisema jinsi anafurahia hatua ya kuwa mzazi na anaridhia sana katika kusaidia ulezi wa mwanawe.

"Hawakuniambia kuwa baba ni jambo la kusisimua hivi, wala la kufurahisha. Kila siku unazidi kumpenda na kumjua mwanao. Nilikuwa ninahitaji kufichua hisia zangu, mwanangu ni bora zaidi. Ni zaidi ya kuwa baba tu, na mimi ni baba bora," mwimbaji wa kibao cha 'In My Bed' alisema.

Vilevile Mdee alisema anachukulia uzazi kama baraka na jambo la kipekee ambalo hawezi kujuta kamwe. 

"Najiskia poa. Kuwa mama ni kitu cha kipekee sana. Natamani mashoga zangu ambao wamewahi kuwa na watoto wangeniambia. Kama wangeniambia kitambo ningesema nakosa kweli, lakini sikuwa naelewa. Ni kitu kigumu kueleza kwa mtu ambaye hajawahi kuwa mama. Imekuwa baraka, nafurahia wakati wote" Mdee alisema.

View Comments